Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa (Mb), akizungumza na wajumbe katika mkutano wa Baraza
la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),
lililofanyika mkoani Kigoma.
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa
(hayupo pichani) katika ufunguzi wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick
Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi akitoa
taarifa ya utendaji kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia), mkoani Kigoma.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Samson Hanga akizungumza na wajumbe katika
mkutano wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS), lililofanyika mkoani humo.
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa baraza la tisa la wafanyakazi wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), wakiimba wimbo wa mshikamano katika ufunguzi
wa baraza hilo, mkoani Kigoma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick
Mfugale (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa katika
Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala huo, lililofanyika mkoani
Kigoma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la
Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani
Kigoma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa (Mb), amewapongeza Wakala wa barabara nchini
(TANROADS), kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika
vituo vya mizani hapa nchini.
Akifungua
Mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma,
Naibu Waziri Kwandikwa, amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji
wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa
ya wote.
“Hakikisheni
kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa hatua za kisheria
anachukuliwa ikiwemo na kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la
rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, amesema Naibu
Waziri Kwandikwa.
Naye
Mtendaji Mkuu Wa Wakala huo Eng. Patrick Mfugale, amesema kuwa katika
kipindi cha mwaka mmoja watumishi 71 wamefukuzwa kazi katika vituo
mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo vya
rushwa.Ameongeza
kuwa TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo
vya mizani vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa
wananchi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia
Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga kutekeleza
kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini kwa
wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.
Wajumbe
wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote nchini wamekutana katika
mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini utendaji kazi
wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya kazi zake
kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment