Baraza
la Habari Tanzania (MCT) limerahani matukio ya uvunjifu wa uhuru kwa
waandishi wa habari ambayo ynaendelea kutokea kutokana na matukio 30 yaliotokea kuhusu hapa nchini.
Kutokana
na matukio hayo MCT itawafikisha mahakamani wote wanaowazuia,
kuwanyanyasa na kuwapiga waandishi wa habari wawapo katika majukumu yao
ya kazi.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga (Kulia)
akizungumza na waandishi wa habari jleo ijini Dar es Salaam.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga
katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Kupinga Jinai Dhidi ya
Wanahabari, yanayofanyika duniani kote na kwamba baraza linachukua hatua
hiyo kutokana na vitendo hivyo kushamiri .“MCT haliridhishwi na mwenendo wa hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini . Inasisitiza kuwa haki ya kupata habari na uhuru wa kujieleza ni haki ya Kikatiba,” amesema Mukajanga.
Akitolea
ukiikwaji wa haki hizo ni katika kipindi cha miezi sita iliyopita
magazeti matano yemefungiwa ambayo ni Mseto, Mwanahalisi, Mawio,
Tanzania Daima na Raia Mwema.
Amesema
mbali na kufungiwa kwa vyombo hivyo, waandishi mbali mbali wamepata
misukosuko wakati wakiwa kazini. Baadhi yao ni Halfani Lihundi wa ITV
Arusha, ambaye aliwekwa kizuizini na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru, Alexander Mnyeti.
Mwingine
ni Augusta Njonji wa Nipashe ambaye hivi karibuni aliandika habari za
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kukamatwa na kuhojiwa na
polisi na baadae kuachiwa kwa dhamana.
Pia
waandishi wa Mwananchi, Azam TV na Mtanzania huko Geita nao walipata
msukosuko wakati wakiwa kazini kuripoti rabsha za wanafunzi wa Sekondari
ya Geita hivi karibuni.
Matukio
mengine amesema ni pamoja na waandishi Joel Maduka wa Storm FM na
Vallence Robert wa Channel Ten kushambuliwa na polisi wakiwa kwenye
msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa huko Geita.
Wengine
ni wapiga picha wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Selean Mpochi na John
Badi, ambao walinyang’anywa kamera zao wakati wakifanya kazi zao katika
mkutano wa Sheikh Ponda katika hotel ya Iris ya jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
Amesema ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa waandishi wa habari amekuwa ni kwa serikali kupitia polisi, wakuu wa mikoa na wilaya.
No comments:
Post a Comment