Hapakazi tu,
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za walimu mkoa wa Dar es salaam.
RC Makonda akifanya akijenga moja ya ofisi za walimu katika shule ya msingi Kichangani
Afisa
Elimu wilaya ya Ilala S .Thomas akitoa salamu za utambulisho katika
eneo la uzinduzi wa zoezi la ujenzi wa ofisi 402 za walimu mkoa wa
Dares salaam uliofanyika katika shule ya msingi kichangani ilipo Majohe
Ilala .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda ,amezindua zoezi la ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Walimu Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kuakamilika ujenzi huo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu mkoa hapo na kuongeza kuwa ujenzi wa Ofisi utafanka kwa haraka, chini ya Vijana wenye morali ya kazi kutoka JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.
Ramani ya ofisi hizo naonyesha kuwa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Walimu wa kawaida, Mhasibu, Karani, Chumba cha kuhifadhi Mitihani, Vyoo vya kisasa, Stoo, Jiko, Chumba cha Mikutano na sehemu kuweka Mafaili ambapo ndani ya ofisi zitafungwa AC, Feni, Samani, Taa za kisasa na Umeme.
Akizungumza Katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na upandaji wa Miti RC MAKONDA amesema kuwa lengo la ujenzi huo ni kuwezesha Walimu kufanyakazi katika Mazingira mazuri yatakayowapa morali na hamasa ya kufundisha Wanafunzi.
Sanjali na hayo Makonda amewapongeza Walimu wa shule za msingi kwakuwezesha Mkoa wa Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Darasa la saba ukilinganisha na nafasi ya nne waliyo pata mwaka jana na na amewaomba kuto kuto ichia nafrasi hiyo ,nakuwataka pia walimu wa shule za secondari nao kujitahidi ili waongoze katika matokeo ya mtihani kitafa.
"Rais ,ameshatuonyesha dira kwa kutoa elimu bure na sisi wasaidizi wake ni lazima tuendeleze maono yake, mimi sio kiongozi wa kusubiri kuagizwa ndio nifanye kazi kama ilivyo kwa Remote hadi ibonyezwe ndio ifanye kazi, mimi ni kiongozi wa kujiongeza, sijachaguliwa kuwa mzigo kwa serikali bali kuleta matumaini kwa wananchi"Alisema.
Amewataka Viongozi kuacha Siasa kwenye mambo ya Msingi yanayolenga kuleta maendeleo kwakuwa Maendeleo hayana chama wala ubaguzi wa Dini.
"walimu hawa wanapowafundisha watoto wetu hawawaulizi vyama vyao wala dinizao tena watoto wenyewe hawa hawana vyama naombambeni ndugu zangu tuwe wamoja katika mambo ya maendeleo ,nashangaa kuna Wilayamoja wao hatakamanijambo jema nikupinga tu ,madai yao eti watanipa kiki,mmi sitafuti kiki nafanya kazi.
Naye Diwani wa kataya Majohe mhe. waziri amepongeza hatua ya mkuu wa koa wa Dar es salaam kwajuhudi anazozifanya katika shuguli za maendeleo na kusema kuwa anamuuga mkono aendelee mbele zaidi.
"kwakweli hatamimi ilikuwa ni shauku yangu kuona walimu wakifanya kazi katika mazingira mazuri wanakuwa naofisi nzuri na anachokifanya Makonda kitukizuri napia kama kiongozi wa serila anatimiza wajibu wake mimi nimtakie kilalakheri" Alisema Diwani huyo.
Nao baadhiya wananchi walihudhuria uzinduzi huo wamesema weshukuru hatua hiyo na kusema kuwa walimu walikuwa wanadharirika ,walidharaulika walikuwa kamawametengwa ukienda ofisi za wizara zingne wanaofisi lakini wao walisahaulika sasa watafanya kazi kwa moyo kwakuwa watakuwa huru na maboyao .
Kwaupande wake Mwenyekti wa kamati ya ujenzi Canal Mbuge amewataka watanzani kuendelea kuchagia ujenzi huo ilikujenga mshika mano na utaifa kwa kujitolea katika mabo ya maendeleo na kuahidi kuwa wao kama wasimamizi wa ujenzi huo watahakikisha ujenzi huo unafanyika kwa ubora na viwango na kukamilika kwa wakati.
Awali mkuu wawilaya ya Ilala mhe. Sophia mjema akizungumza wakati wa ukaribisho amemshukuru Rc Makonda kwa moyo wake wa kuwajali walimu kwa kuona shida yayao na kuahidi kufanya naye kazi begakwabega i kuendelea kutatua kero za wali na wananchi kwa ujumla ,Uzinduzi huo umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Lazolo Mambosasa, Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu, Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule ,Diwani, Pamoja na wanachikutoka maeneombalimbali ya wilaya Ilala.
No comments:
Post a Comment