Na.WAMJW.Dodoma
Taasisi
ya Chakula na lishe nchini imetakiwa kujikita katika kutoa elimu kwa
umma ili wananchi waweze kujua faida ya kula chakula bora na kuepukana
na utapiamlo na udumavu
Hayo
yamesemwa na Mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya
jamii Mhe. Peter Serukamba wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya
utendaji wa shughuli za taasisi hiyo mjini Dodoma leo.
Mhe.Serukamba
alisema bila elimu kwa umma wananchi watakuwa wanatumia fedha nyingi
kwa ajili ya matibabu kwa kuwa hali ya udumavu ni mkubwa ,”watu wakiwa
na chakula na lishe bora unakuwa na uhakika hutougua hovyo na kupoteza
fedha nyingi kwa ajili ya matibabu,lakini wakijua wale mlo gani ambao ni
sahihi hii itasaidia kutokomeza kabisa tatizo hili”
Aidha,
alisema Tanzania haina tatizo la chakula ila hawafahamu ni mlo gani
sahihi wanapaswa kula hivyo kwa kutoa zaidi elimu itakua ni kinga na
itasaidia wananchi wasiugue
“Taasisi
hii iboreshwe na mkishirikiana na Tamisemi,wakulima na wasafirishaji wa
mazao kupitia maofisa maendeleo ya jamii mtawafikia wananchi wengi na
hakutokuwa na vizazi vyenye udumavu na matatizo ya akili.
Awali
akiwasilisha taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto dkt.Faustine Ndugulile
alisema zaidi ya asilimia 35 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya
miaka mitano nchini vinachangiwa na matatizo ya lishe duni na katika
kipindi cha mwaka 199 hadi 2015/2016 vifo vya watoto vimepungua kutoka
147 hadi 67 kwa kila vizazi hai 1000.
“Serikali
inafanya jitihada kubwa katika kumjenga mtoto ili akue vizuri kimwili
na kiakili kuanzia siku elfu moja za mwanzo za mtoto ambazo ni muhimu
kwa makuzi ya mtoto”.
Hata
hivyo dkt.Ndugulile alisema hali ya lishe nchini inaendelea kuimarika
kutokana na kupungua kwa viwango vya utapiamlo nchini kati ya mwaka 1992
na 2015.
Alisema
udumavu (urefu wa umri) umepungua kutoka asilimia 49.7 hadi 34.4 na
mikoa inayoongoza ni Rukwa (56%) na Ruvuma (44%) ,kwa upande wa ukondefu
(uzito kwa urefu) kutoka asilimia 7.8 hadi 4.5 na mikoa inayoongoza ni
Zanzibar-Kusini Pemba na Kaskazini Pemba(9%),Manyara (6.4%),Geita
(6.2%),Kigoma (6%) na Morogoro (6.0%)
Kwa
upande wa uzito pungufu alisema (uzito kwa umri) kutoka asilimia 25.1
hadi 13.7 na mikoa inayoongoza ni Rukwa (23%),Arusha (20%) pamoja na
Kigoma (20%).
Vilevile,mwanamke
mmoja kati ya kila wanawake 10 walio katika umri wa kuzaa ana uzito
pungufu (underweight) wakati asilimia 18 wana uzito mkubwa (over weight)
na asilimia 10 wana kiribatumbo(obesity).Mikoa inayoongoza kwa
kiribatumbo ni Zanzibar mjini Magharibi kwa 22%,Unguja Kusini 19%,Dar es
Salaam 21%,Kilimanjaro 19% na Tanga 17%.
Naibu
Waziri huyo aliahidi kuwa watajipanga katika kutoa elimu ya afya kwa
umma na kuwafikia wananchi wengi zaidi “bado Watanzania hawajui kula
lishe iliyokamilika na matumizi bora ya chakula.
No comments:
Post a Comment