NA BASHIR NKOROMO
MBUNGE wa Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, amesema ameridhishwa na kiwango cha ujenzi wa Barabara ya Olympio, katika kata Upanga Mashariki, huku akilalamikia ujenzi wa Barabara ya Mtaa wa Mfaume ambayo ujenzi wake umekwama.

Zungu amesema hayo leo alipokagua maendeleo ya ujuenzi wa barabara hizo
ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami chini ya usimamizi na gharama za
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
“Kama mnavyoiona, barabara hii ya Olympio inayojengwa na kampuni ya
kigeni ya China Railway Seventh Group (CRSG), imejengwa kwa kiwango
kizuri kabisa, lakini hii ya Mtaa wa Mfaume yenye urefu wa mita 900,
ambayo mkandarasi wake ni kampuni ya CASCO abayo ni ya mzawa mwenzetu
imekwama kumalizika, Sasa tunamtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri tujue
nini hasa kimesababisha ujenzi wa barabara huu kukwama”, amesema Zungu.
Amesema, wakati barabara ya Olympio yenye urefu wa mita 740 ujenzi wake
umekamilika kwa kiwango kikubwa tangu Septemba 30, mwaka huu, ujenzi wa
barabara ya Mfaume umekwama hadi sasa kutokana na Mkandarasi
kusimamishwa kuendelea kutokana na kuonekana anaijenga kwa viwango vya
chini.
Wakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG Zhou
Cunfei, alisema licha ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 95, kampuni hiyo
inamalizia sehemu chache zilizobaki na inainatarajia kuikabidhi rasmi
Januari 2, mwakani.
Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza alipokagua ujenzi wa
Barabara ya Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Watatu
kulia ni Wakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou CunfeiWakala wa Ujenzi wa barabara ya Olympio kutoka kampuni ya CRSG ya China Zhou Cunfei akizungumzia wakati Zungu alipokagua ujenzi wa Barabara hiyo, leo.
Mbunge
wa Ilala Mussa Azan Zungu akikagua ujenzi wa Barabara ya
Olympio, Upanga Mashariki jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia niWakala wa Ujenzi wa barabara hiyo kutoka kampuni ya CRSG ya China, Zhou Cunfei

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Upanga Mashariki, akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo ya Olympio
No comments:
Post a Comment