Gari
la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema limechomoka matairi
leo Jumatatu baada kudaiwa kuwa limefunguliwa nati 13 kati ya 20 na
watu wasiojulikana.
Lema
amesema walikuwa wamepanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema),
Joshua Nassari kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam
kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema.
Hata hivyo amesema majira ya mchana alipokuwa na gari alihisi mlio kwenye tairi ndipo alikwenda kuliegesha hoteli ya Equator.
Amesema
kutokana na kulitilia shaka gari aliomba lifti kwenye gari la
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es
Salaam.
"Asubuhi
leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli
alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka,"
amesema.
Amesema
tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba
kampuni ya ulinzi ya inteligence inayolinda nyumba yake kufanya
uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.
No comments:
Post a Comment