Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari (Hawapo kwenye
picha) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa tukio la kupokea
mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe mweupe,
pembeni ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akipokea msaada wa mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa Mratibu
wa Utepe Mweupe Bi.Rose Mlay wakati wa tukio lililofanyika mapema leo
katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa tukio la kupokea mashine ya
kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe mweupe lililofanyika
mapema leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
akiongea na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa kupokea
msaada wa mashine ya kutoa dawa ya usingizi kutoka kwa taasisi ya Utepe
mweupe mapema leo jijini Dar es salaam, pembeni ni Mratibu wa Utepe
Mweupe Bi.Rose Mlay.
NA NOEL RUKANUGA
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imepokea msaada wa
mashine ya kutoa usingizi wakati wa upasuaji yenye thamani ya zaidi ya sh.
milioni 60 kutoka Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ).
Akipokea msaada huo Waziri wa afya, Maendeleo ya
Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema kuwa mashine hiyo itakuwa na
msaada mkubwa katika ikupunguza vifo vya watoto na akina mama wakati wa
kujifungua.
Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zimebainisha
kuwa wanawake 30 hufariki kila siku jambo ambalo sio rafiki kwa taifa.
Mhe. Ummy amesema kuwa katika kuhakikisha
wanaboresha mazingira ya huduma za afya kwa wazazi na watoto, serikali
imejipanga kabla ya mwezi Juni mwakani kuongeza vituo 170 vya kutoa huduma ya
uzazi.
Amefafanua kuwa serikali imetenga sh.bilioni 8 kwa ajili ya kununua vifaa
pamoja na dawa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ili kukabiliana na vifo
vya akina mama na watoto.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Dk. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa mashine hiyo inauwezo wakutengeneza
asilimia 21 ya hewa ya oksijeni kwa ajili ya kumsaidia mgonjwa.
Dk. Ulisubisya amesema kuwa mashine hiyo inawezo mkubwa
kutokana inaweza kufanya kazi bila kutumia umeme wa kawaida.
“Umeme unapokatika ina uwezo wakutumia hewa ya
oksijeni ya kawaida ambayo inatumiwa na watu wengine” amesema Dk. Ulisubisya.
Ameeleza kuwa msaada huo ni hatua kubwa katika maendeleo ya uboreshwaji wa
huduma za afya nchini, kinachotakiwa kwa sasa ni kuandaa wataalamu wakutumia
mashine hiyo.
Naye Mratibu wa Taifa wa WRATZ Rose Mlay, amesema
kuwa ni kuhakikisha wanaokoa maisha ya wazazi na watoto wakati wa kujifungua.
Amesema wameona ni vema kufanya hivyo ili
kuhakikisha katika sekta ya afya inasonga mbele na kuwa na mafanikio.
“Mashine hii itatumika kusaidia kuokoa maisha ya
mama na mototo na watu wengine” amesema Mlay.
No comments:
Post a Comment