A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 29, 2017

RC MAKONDA: WADAU JITOKEZENI KUUNGA MKONO UJENZI WA OFISI ZA WALIMU


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Mifuko 10,000 ya Saruji iliyotokana na kiasi cha Million 100 ya awali iliyotolewa na Bank ya CRDB kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu.

Akizungumza kwenye Ghala la kuhifadhia vifaa vya ujenzi wa Ofisi hizo lililopo kwenye Kambi Mama ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Mgulani RC Makonda ameishukuru Bank ya CRDB kwa kutoa fedha zilizofanikisha kupatikana kwa mifuko hiyo.

Aidha amesema Bank ya CRDB pia imejitolea kuweka Dawati maalumu kwenye kila Tawi la Bank hiyo kwaajili ya wananchi wanaotaka kuchangia Ujenzi wa Ofisi za Walimu ambapo Mwananchi anaweza kuchangia kiasi chochote cha Fedha ambapo wengine wataweza kuchangia kwa SimBank

Amesema kuwa kazi ya ujenzi wa Ofisi za kisasa za Walimu iyafanyika Usiku na Mchana chini ya Vijana wenye morali ya kufanya kazi kutoka JKT,Jeshi la Magereza na Jeshi la Polisi ambao Wamemuunga Mkono RC Makonda.

Makonda amewapongeza wadau waliomuunga mkono na wanaoendelea kumuunga mkono katika kufanikisha kampeni hiyo ambapo amewaomba Wananchi kumuunga mkono.

Amesema kuwa hadi sasa amefanikiwa kupata wadau walioahidi kufunga miundombinu ya vifaa vyote vya umeme ikiwemo Taa, Feni ambapo wengine wametoa Mabati 10,000 huku wengine wamejitolea kuweka Vifaa vyote vya Vyoo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages