Rubani wa shirika la ndege la Etihad amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kurusha ndege ya mizigo ya shirika hilo.
Rubani huyo aliyekuwa anaendesha ndege ya mizigo yenye namba EY927 ya
shirika la Etihad alishikwa na homa ya ghafla kitu ambacho kiliirazimu
rubani wa pili kufupisha safari hiyo kutoka Abu Dhabu kwenda Amsterdam
na kulazimika kutua Kuwait kwa dharula.
Shirika hilo la Etihad limethibitisha taarifa hizo kupitia kwa msemaji
mkuu wake ambaye hata hivyo hakutaja jina la rubani, umri wala uraia
wake.
“Baada ya kampteini wetu kudondoka ghafla ilimlazimu rubani wetu
msaidizi kufanya mawasiliano ya haraka ili kuweza kutafuta msaada wa
kutua nchini Kuwait, tumesikitishwa na kifo chake na kampuni yetu
inaungana na familia yake kuwafariji“,imeeleza taarifa iliyotolewa jana
(Jumatano) na shirika hilo kupitia kwa msemaji wa kampuni ya Etihad.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni miezi sita tu imepita tangu rubani wa
ndege wa shirika la ndege la Marekani kuumwa ghafla na kulazimika ndege
hiyo kutua kwa dharula.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Rubani wa shirika la Etihad afariki dunia ghafla ndege ikiwa angani
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment