Makamu
wa Rais wa Itel Mobile Bw.Lesley Ding akizungumza na wadau pamoja na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho
ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.hafla hiyo hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Itel Mobile Tanzania,Irene Uwoya akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa
habari wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya
Kampuni hiyo.
Burudani ikiendelea katika hafla hiyo

Wadau waliofika katika maadhimisho hayo jijini dar es salaam.
………………………
Kampuni
ya Simu ya Itel Mobile imetimiza madhamisho ya miaka 10 tangu
kuanzishwa kwake huku ikiendelea kufanya vizuri katika soko la mauzo ya
Simu na kuwa kinara kwa ubora wa bidhaa zake barani Afrika na nje ya
Afrika.
Miaka
10 iliyopita Itel Mobile ilizindua mpango wa kumwezesha kila mmoja kuwa
na simu bora kwa ajili ya mawasiliano ya uhakika,katika kipindi hicho
chote tumepitia katika kipindi kigumu katika Nyanja za kiuchumi na
kisiasa lakini tumeweza kufanikiwa kutimiza mlongo mmoja kwa uthabiti
mkubwa.
Itel
Mobile iliingia kwenye soko la Afrika mwaka 2007 na baada ya kuanzishwa
kwa timu ya watu wenye ujuzi na moyo wa kufanya kazi na mpaka sasa
miaka 10 kampuni hii imekuwa na kuweza kuenea zaidi ya nchi 45 Duniani
kote.
Ndani
ya miaka 10 Itel Mobile imekuwa na mabadiliko makubwa chanya ya bidhaa
kutokana na kufuatwa matakwa ya wateja wake hivyo imepelekea kupendwa na
kuleta mvuto kutokana na kuboreshwa kwa bidhaa hizo kwa ubunifu mkubwa.
”Tumeweza
kuongeza idadi ya wateja mara mbili zaidi barani Afrika na pia shukrani
zetu za dhati ziende kwa wateja wetu pamoja na mashabiki wote wa Itel
na mpaka sasa tumeuza jumla ya simu milioni 100’alisema Makamu Rais
Aidha
nguvu kubwa yetu inatokana na bidhaa zetu zilivyo bora pamoja na timu
ya wafanyakazi wetu ambao kila mmoja amekuwa akijituma kutokana na
nafasi yake na pia ubora na mvuto wa bidhaa unatokana na mapendekezo ya
watumiaji wetu na huduma za matengenezo baada ya mauzo na warantii ya
miezi 12 kwa bidhaa zetu zote.
Hata
hivyo tumekuwa na ushirikiano na mastaa wa nchi za Afrikia kama
mabalozi wa kampuni yetu na wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu
na uelewa kuhusu kampuni ya Itel ambapo imekuwa kampuni 3 bora barani
Afrika.
Na
kwa kuonesha upendo wetu Afrika tumekuwa tukifanya matendo ya ukarimu
kwa jamii na kujitolea kutembelea baadhi ya shule na vituo vya watoto
yatima kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira
magumu.
Itel
Mobile Tanzania kwa kushirikiana na balozi wa kampuni mwaka huu peke
mpaka sasa tumewasaidia katika mahitaji muhimu zaidi ya watoto 400
wanaotoka mazingira magumu wakiwemo yatima na tunaendelea kuunga mkono
jitahidi za kusaidia jamii.
Tunaposherekea
miaka 10 tunatarajia kuleta mabadiliko makubwa zaidi ili kuimarisha
bara la Afrika kwa kutoa bidhaa bora za mawasiliano na leo tunazindua
simu mpya ambazo ni za kisas zaidi yaani Itel S12 na S32 na zina ubora
kutokana na kuwa kila simu simu ina kamera mbili za mbele pia mwonekano
mzuri na kusaidia kuchukua selfie ya kundi ambayo ina uwezo wa kuchukua
watu wengi zaidi pia zina Fingerprint ‘alama za vidole’.
No comments:
Post a Comment