Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 30 Septemba, 2017
amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika
kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na
Serikali katika kupambana na Ujangili kwa kutoa taarifa za siri
zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.
“Ili
kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na
vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika
mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini
tuambieni tutamshukia kama mwewe” alisisitiza Prof. Maghembe.
Ufunguzi
huo wa Siku ya Utalii Kitaifa umeenda sambamba na ufunguzi wa Maonesho
ya Karibu Kusini pamoja na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo
SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini
kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja
na watoa huduma hiyo.
Alisema,
kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii
Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya
Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi
wa Viwanda”.
Alisema
sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa
kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato
cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine.
"Utalii
ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni
kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na
asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe.
Alisema
mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani
milioni 1,353.29 mwaka 2011 hadi Dola za Kimarekani milioni 2,131.57
mwaka 2016.Alisema
mchango huo umechagizwa na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi ambao
waliongezeka kutoka 867,994 mwaka 2011 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016.
Hata
hivyo, alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi
za Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya
rasilimali, utangazaji, mazingir bora ya uwekezaji na ushirikiano
madhubuti baina ya sekta ya umma na binafsi.
Kila
mwaka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani huadhimisha Siku ya
Utalii tarehe 27 Septemba kwa lengo la kuhanasisha umuhimu wa sekta hiyo
katika kuleta maendeleo ya jamii, utamaduni, kukuza demokrasia, kutunza
na kuhifadhi mazingira, kujenga uchumi na kuimarisha mahusiano ya
kitaifa na kimataifa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati), Naibu
Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza (kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya
Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kauli
Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii
Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya
Uchumi wa Viwanda”.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa
Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini
mkoani Iringa jana. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 2, Oktoba. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Iringa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iirnga, Richard Kasesela akiratibu shughuli nzima ya maadhimisho hayo.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao
umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii
wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na
Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,
Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi
Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu
kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip
Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa
maadhimisho hayo.
Baadhi ya Machifu wa Iringa waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatila ufungunguzi wake.
Sehemu
ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho
ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri,
Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela
wakielekea kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Kichangani
Mkoani Iringa jana.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akipimwa afya katika
banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya
Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), akikagua bidhaa za
wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya
Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa pili
kushoto).
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimuonyesha Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza moja ya bidhaa za wajasiriamali wakati
wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani
na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wengine pichani ni
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) na Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia). Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akikagua kifaa
maalum cha kuwashia umeme katika banda la VETA wakati wa zoezi la
kukagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho
ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya
Iringa, Richard Kasesela (kushoto).
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), Naibu
Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) wakipata maelezo katika
banda la Sido kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini
yanayoendelea Mkoani Iringa.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), akikagua gari
maalum kwa ajili ya mafunzo katika banda la VETA wakati wa zoezi la
kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho
ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wanaoshuhudia pichani ni Mkuu wa
Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa,
Richard Kasesela (wa tatno kulia).
Naibu
Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Waziri wa Maliasili,
Prof. Jumanne Maghembe (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza wakikagua vifaa vya mfumo wa umwagiliaji vilivyotengenezwa na
VETA katika maadhimisho hayo.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akisalimiana na
Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii
Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akionesha picha za nyayo za
Zamadamu wa Laetoli na Engaresero zilizogundulika Ngorongoro mkoani
Arusha takribani miaka milioni 3.6 iliyopita kufuatia tafiti mbalimbali
zilizofanyika kwa muda mrefu.
Katika maadhimisho hayo kuna fursa za kuwaona wanyamaori mbalimbali ikiwemo Simba kama wanavyoonekana kwenye banda lao maalum.
No comments:
Post a Comment