Jumla
ya Kampuni 126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano
zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la
hifadhi ya jamii NSSF mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango
ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa
NSSF mkoani Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo
yamegawanyika kati ya waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi
milioni 50 na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia milioni 5 hadi
49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi elfu
ishirini hadi milioni 4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao
inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.
“Waajiri
wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za
kimahakama zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017
mtawajua ni waajiri gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi
gani wanadaiwa kila mmoja wao” alisema dokta Maduga
Amesema
kuwa Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha
michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita,
kitendo hicho kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi
wao kwa kukosa huduma za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya
wanachama taarifa zao za kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda
ule ambao michango haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa
mawazo kwa wafanyakazi husika.
Mwanachama
ana haki ya kulipwa michango yake yote akiacha kazi au kampuni ikifa na
kuacha kuendesha biashara hulazimika kulipa fedha zote za michango ya
wanachama na wao kama taasisi inayosimamia haki za waajiriwa huhakikisha
malipo yote yanalipwa na kutolea mfano kampuni za snowcrest na mukidoma
zilizositisha shughuli zake na kutangaza kufilisika walihakikisha kuwa
kila mfanyakazi anapata mafao yake bila wasiwasi wowote.
Amesisitiza
kuwa mwanachama akishaacha kazi atasubiri kwa kipindi cha miezi sita
ndiyo aweze kupewa fao la kustaafu na kipindi hiki huwekwa ili kumpa
nafasi mwanachama kuweza kutafuta kazi na ama kuajiriwa na kampuni
nyingine na changamoto inayowakabili ni kuwa baadhi ya wanachama hufoji
barua za kuacha kazi ili waweze kupewa mafao yao huku bado wanafantya
kazi jambo ambalo halikubaliki kwa mwanachama kulipwa fao lake huku
anafanya kazi.
Naye
Straton Simon Afisa msimamizi wa fao la matibabu NSSF kanda ya
kaskazini inayowakilisha mikoa ya ARUSHA,KILIMANJARO, TANGA na MANYARA
amesema kuwa fao la matibabu hutolewa bure na mfuko huo kwa kila
mwanachama anayekuwa amewekewa michango yake kwa miezi mitatu na
kuendelea na fao hili halihusiani na kukatwa akiba yako siku
utakayostafu kazi au kampuni yako kusimama kufanya kazi hivyo amewataka
wanachama wasiwe waoga kutumia fao hili kwani lina faida kwa mwanachama
na wategemezi wake wane ambao ni mke au mume na watoto wane.
Amesema
kwa Arusha pekee NSSF ina mkataba wa matibabu kwa wanchama wake na
hospitali 34 zinazotibu wanachama wote wa hiari na wale waajiriwa ambao
mpaka sasa wanafikia 18,400 na kwa kanda nzima ya kaskazini wanafikia
wanachama 34000 wanaopata fao hilo la matibabu na kuwasihi wanachama
wengine wote wahakikishe wanajaza fomu na kuchagua moja ya hospital
ambayo ungependa kutibiwa kati ya hizo hospitali 34 ili wanufaike na fao
hilo muhimu kwa maisha ya mwanachama.
No comments:
Post a Comment