Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amepiga marufuku Shule zote
Mkoani Singida kuagiza chaki nje ya Mkoa kwakuwa kuna viwanda
vinavyozalisha chaki bora mkoani hapa.
Dkt
Nchimbi ametoa katazo hilo mara baara ya kufanya ziara katika viwanda
viwili vinavyozalisha chaki katika halmashauri ya Itigi na kushuhudia
chaki yenye ubora ikiwa imezalishwa kwa wingi na ikiwa haijapata soko.
“Hawa
wenye viwanda wamejitahidi kuzalisha chaki bora haina vumbi na inauzwa
kwa bei sahihi lakini shule zetu badala ya kuja kununua hapa ambapo ni
karibu wanaagiza Dar es salaam na mikoa mingine”, amesema na kuongeza
kuwa,
“Yani
mnasubiri chaki hii hii iende Dar es Salaam halafu mnainunulia kutoka
huko, hii haikubaliki, kuanzia leo shule zote zinunue chaki hapa hapa
ili tupunguze gharama pamoja na kuinua viwanda vyetu”.Dkt
Nchimbi ameongeza kuwa Mikoa ya Jirani itakayonunua chaki katika
Viwanda vya Singida, vitasafirishiwa chaki hiyo bure kama motisha kwa
kuunga mkono viwanda hivyo.
Amezitaka
halmashauri kushirikiana katika kuboresha mazingira ya utendaji wa
viwanda hivyo hasa kwa kuangalia namna ya kuboresha barabara zinazoenda
katika machimbo ya jasi yanayotumika kutengeneza chaki kwakuwa wenye
viwanda wamekuwa wakilalamikia ubovu wa barabara hizo.
Aidha
Dkt Nchimbi ametoa wito kwa wenye viwanda wote nchini ambao wanatumia
madini ya jasi (gypsum) katika shughuli zao wasihangaike kutafuta madini
hayo bali waje singida kuna viwanda vinatengeneza madini hayo kwa ubora
mzuri na bei nzuri.
Amesema
viwanda vya kutengeneza jasi Singida vimekuwa vikizalisha madini hayo
kwa wingi hivyo wenye uhitaji wa madini hayo kutengenezea chaki, gypusum
board POP, wanakaribishwa kununua madini hayo mkoani hapa.
Dkt
Nchimbi amewapongeza wenye viwanda hivyo kwa kutumia rasilimali kama
madini ya jasi iliyopo Singida kwa kuanzisha viwanda mabavyo
vinatengeneza ajira na kukuza uchumi kwa kuwa wao wamekuwa walipa kodi
wazuri.
Naye
Meneja wa kiwanda cha chaki cha Dober Color kilichopo Itigi Abdul
Mahamoud amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hatua yake ya kukataza kuagizwa
chaki nje ya Singida kwakuwa kutaongeza soko ambalo litasaidia viwanda
hivyo kukua.
“Mkuu
wa Mkoa tunashukuru kwa katazo hilo kwakuwa litafanya viwanda vyetu
vikue na kuongeza uzalishaji, lakini pia itafanya viwanda hivi viongeze
ajira na hata kodi tunayolipa itaongezeka hivyo kukuza uchumi wa
Singida”, amesema Mahamoud.
Ameongeza
kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinazalisha tani hamsini kwa siku lakini
kutokana na katazo hilo matarajio ni kuongezeka uzalisha hadi kufikia
tani 200 za chaki kwa siku.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akishiriki zoezi la kutengeneza
chaki katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya
Itigi.
Mkuu
wa Wilaya ya Manyoni Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amebeba ili kuzianika
chaki alizotengeneza Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika kiwanda cha
Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua kiwanda cha kutengeneza
jasi cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Dober Color wakifungasha chaki, Meneja wa Kiwanda hicho
amesema sehemu ya kufungasha chaki hiyo inafanywa na wanawake kwakuwa
wako makini na haraka.
Mkuu
wa Mkoa Singida Dkt Rehema Nchimbi akikagua ubora wa chaki
inayozalishwa katika kiwanda cha Dober Color Kilichopo Halmashauri ya
Wilaya ya Itigi, kushoto kwake ni Meneja wa Kiwanda hicho Abdul Razak
Mahamoud.
No comments:
Post a Comment