Kamishna
Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka
kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa
wa Kagera Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia katika kijiji cha
Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa
Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo
vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia
Tanzania.
Baadhi
ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya
Karagwe Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya
Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya
wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu
ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala alitoa wito kwa wanakijiji
hao kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na
kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna
mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment