Kampuni
yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya
Dar es Salaam (DTBi) imeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa waalimu
katika maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo
hayo kwa waalimu yameanza kufuatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa
mafunzo hayo na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za
msingi,sekondari, vyuo vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na
kufaidika na mafunzo haya yatakayowasaidia kuvumbua application
mbalimbali, kuwapatia vijana ujuzi katika mswala ya Tehama na pia
kuwawezesha vijana wajasiriamali kuendesha shughuli zao za kibiashara
kwa kutumia technologia za kisasa.
Akiongea kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde alisema,
‘Hapo
awali tulikuwa tumeanza kutoa mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi lakini
tumeona ni bora na waalimu wa hapa shule hii Kijitonyama nao waanze
kupata mafunzo. Hii itasaidia kwani kwa baadae ndio watakaokuwa wakitoa
mafunzo kwa wanafunzi na hii itatupa nafasi ya kuendelea kuwezesha shule
zingine.
Waalimu
wamepokea hatua hii kwa furaha na wanao hamasa kubwa kwenye mafunzo.
Hii inathibitisha nia ya kampuni ya Airtel ya kutoa fursa kwa kila
Mtanzania, aliongeza Matinde.
Hata
hivyo, Matinde alisema kuwa mafunzo kwa wanafunzo ambao walikuwa
washaanza yataendelea vile vile. ‘Utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wale
wanafunzi ambao walikuwa washaanza utaendelea vile vile. Kilichofanyika
ni chukua hatua ya ziada ya kuwapa walimu mafunzo ya Tehama ili nao
waweze kuwa kwenye nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi hawa’ alisema
Matinde.
Matinde
aliongeza kuwa bado tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa
vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara
kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani
vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama
kwa ujumla.
Kwa
upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “
Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa walimu wa shule ya Kijitonyama.
Tuhahakisha kuwa walimu wamepata mafunzo na kuelewa kabisa ili nao
waanze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi.
Jengela
alisema mafunzo hayo ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji
kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”
msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali.
Bado tunapokea maombi, Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia www.teknohama.or.tz na www.a irtelfursa.com au kwa kutembelea maabara iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama
No comments:
Post a Comment