Muigizaji wa Filamu Bongo, Faiza Ally amefunguka kuupa zaidi muziki wa Alikiba kuliko ule wa Diamond.
Faiza amesema hayo katika mahojihano na TBC Fm kwa kueleza kuwa Diamond
ni mburudishaji wa jumla aliyeleta mapinduzi ya kimuziki lakini Alikiba
muziki wake ni bora zaidi.
“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Alikiba, naupenda sana muziki wa
Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko wa Diamond,” amesema Faiza na
kuendelea.
“Diamond ni ile full Entertainment ukimwalia tu unatabasamu lakini Kiba
ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa muziki akaupa heshima
mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona
kwenye hali ya tofauti ni Diamond,” amesema.
Ikumbukwe kuwa September 3 mwaka huu Faiza aliandika ujumbe katika
mtandao wa Instagram na kueleza kuwa kumpenda Diamond ni jambo la
lazima na sio ombi kutokana na mengi mazuri aliyofayanya katika muziki
wa Bongo Flava.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, September 28, 2017
Faiza Ally afungukia mziki wa Alikiba na Diamond
Tags
BURUDANI#
Share This
About kilole mzee
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment