Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyeshika
mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kitabu cha Mwongozo kwa
Wanamipango (Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo
ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (katikati),
akionesha kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo
la Pili, baada ya kukizindua rasmi katika Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini-Dodoma. Wa pili kushoto ni Kaimu Balozi wa Uholanzi
hapa nchini, Bi. Lianne Houben, na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza
la Uongozi la Chuo hicho Prof. Razack Lokina.
Kaimu
Balozi wa Uholanzi hapa Nchini, Bi. Lianne Hauben (kushoto), akifurahi
wakati akikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb), nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners
Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini, Prof. Razack Lokina, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa
wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua
rasmi mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen
Mayaya, nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners
Handbook), Toleo la Pili, mara baada ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb),
akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,
Kituo cha Kanda ya Ziwa, Dkt. Benedict Kilobe, nakala ya Kitabu cha
Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, mara baada
ya kukizindua rasmi mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi
Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Vedastus Timothy,
nakala ya Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners handbook), Toleo
la Pili, kilichozinduliwa katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini, mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwaongoza
wadau mbalimbali kunyanyua nakala ya kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango
(Planners handbook), Toleo la Pili, kilichoandikwa na Chuo cha Mipango
ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya
nchini Uholanzi (ISS), tukio hilo limefanyika katika Chuo cha Mipango
ya Maendeleo Vijijini, Kampasi ya Dodoma.
Mhadhiri
Mstaafu wa Taasisi ya Kimataifa inayotoa elimu ya masuala ya kijamii
(The International Institute of Social Studies (ISS), kutoka nchini
Uholanzi, Prof. Leo de Haan, akitoa mhadhara kuhusu masuala ya umuhimu
wa mipango katika jamii kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa Kitabu cha
Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook), Toleo la Pili, tukio
lililofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
(katikati-walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa viongozi
wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na wahadhiri kutoka
Taasisi ya Elimu ya masuala ya Jamii (ISS) ya nchini Uholanzi, baada ya
uzinduzi wa Kitabu cha Mwongozo kwa Wanamipango (Planners Handbook),
Toleo la Pili, tukio lililofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini-Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Dodoma
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha
Mwongozo kwa Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango
ya Maendeleo Vijijini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya
nchini Uholanzi (ISS), na kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini
kuandaa mipango yenye tija itakayoiwezesha jamii kuondokana na
umasikini.
Dkt.
Kijaji ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza
uchumi wa nchi ni kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango
shirikishi itakayochangia kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze
kujikwamua kiuchumi.
“Ni
matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo
kwa wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya
kupeleka maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa
wataalamu waliobobea ili kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt.
Kijaji
Ameeleza
kuwa maudhui ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia
Serikali za Mitaa ili watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna
bora ya kupanga mipango yao ya maendeleo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini, Prof.
Hozen Mayaya, amesema kitabu hicho kimelenga kuwaongezea ujuzi wataalamu
wa mipango kwa kuzingatia vitendo zaidi badala ya nadharia.
“Kitabu
cha Mwongozo kwa wanamipango kitakuwa rejea ya nadharia nyingi na njia
ambazo wataalamu wanapaswa kuzijua, namna ya kutekeleza majukumu yao kwa
ufanisi na kuifanya mipango iweze kutekelezeka kama ilivyokusudiwa”
alisema Prof. Mayaya.
Nae
Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Bi. Lianne Houben, ambaye kwa
namna moja au nyingine nchi yake imefadhili uandishi na uchapaji wa
mwongozo huo, toleo la pili, amesema nchi yake inajivunia uhusiano imara
uliodumu kwa miongo kadhaa na Tanzania.
Alisema
kuwa mtazamo wa ushirikiano wake na Tanzania kuanzia mwaka huu ni
kujikita zaidi katika uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na kwamba
uwekezaji wao mkubwa utalenga pia kuboresha kilimo na usalama wa
chakula.
“Uholanzi
ni nchi ya pili katika kufanya biashara na Tanzania ikitanguliwa na
Marekani ambapo mwaka 2016, Uholanzi, imenunua bidhaa zenye thamani ya
Euro bilioni 85” aliongeza Bi. Houben
Aidha,
alieleza kuwa nchi yake imetoa mchango mkubwa katika kuendeleza
rasilimali watu ambapo hadi sasa wanafunzi na wataalaamu katika fani
mbalimbali wapatao 5,000, wamepata mafunzo kutoka katika vyuo mbalimbali
nchini Uholanzi.
No comments:
Post a Comment