A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, August 11, 2017

RC: MAKONDA : KUSAIDIA WALEMAVU KUPATA MIGUU YA BANDIA BURE


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa miguu, wanao hitaji Miguu ya bandia  kwenda kujiandikisha ofisini kwake ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

Mhe. Makonda Ameyasema hayo jana ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa huduma hiyo itakuwa ikitolewa bure kwa wananchi wake kwa kuwa huenda Kuna baadhi ya watu wanahitaji ila hawakuwa na uwezo wa kumudu kununua miguu hiyo ya bandia.

"Nawaomba wananchi wangu mje siku ya jumatatu mjiandikishe na kupima kila mtu mwenye uhitaji huo ili tuweze kujuakipimo cha mguu wako Kabla  ya kutengenezewa, tutakuwa na miguu aina mbili waliovunjika kuanzia kwenye paja na walio katwa  kuanzia chini zaidi ya hapo " amesema Makonda

Amesema, amepewa kazi ya kuhudumia wananchi makundi yote katika jamii na Mhe. Rais Magufuli anataka kila mwananchi  wa mkoa huo aweze kufaidika na Serikali yake.

"Kuna watu wamekatwa miguu kwa ajali mbalimbali hawana uwezo tena wa kufanya shughuli zao lakini tukiwapatia miguu ya bandia wataweza kurejea katika hali ambayo itawawezesha kufanya shughuli zao za kujipatia kipato" amesema Makonda.

Akizungumzia gharama ya miguu hiyo bandia Makonda amesema, miguu hiyo ina gharimu zaidi ya  shilingi milioni 800

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages