Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limejipanga kuanza kutekeleza kwa vitendo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mradi mkubwa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleni Tanga kwa kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi watakaotaka kuzitumia fursa hizo. Mradi huo mkubwa uliosainiwa mwezi mei mwaka huu na kuwekwa jiwe la msingi hivi karibu na Rais John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda unalenga kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi Beng’i Issa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwisho mwa juma, kwamba wamejipanga kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za ujenzi wa maradi huo kuanzisha shughuli za kiuchumi. “Tuejipanga vizuri katika kuwaelimisha, kuwaonesha fursa zitakazo kuwepo na kuwapa uwezesha kupitia mifukoa ya uwezeshaji 19,” serikai imeweka fedha katia mifuko hii hivyo waahitajika kuchagamikia,aliongeza kusema Bi. Issa. Alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutoa fursa za ajira 10,000 na baada ya hapo kutakuwa na ajira 1,000 kwa watanzania, na pia amezitaka Taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA kuendelea kuandaa vijana watakao endana na fursa za ujenzi huo. Bi. Issa alizitaja shughuli za kiuchumi zinatarajiwa kuwepo katika mradi huo ni biashara za usafirishaji wa bidhaa na watu, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huduma za chakula, uuzaji wa bidhaa za chakula, ulinzi, uuzaji wa vifaa vya ujenzi. Zingine ni huduma zingine ni kama vile afya, sheria, fedha, bima, huduma za taka, huduma ukarabati na vifaa vya usalama kazini. Alifafanua kwamba baraza litashirikiana na mikoa ambayo bomba hili linapita kama vile Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na wilaya 24 na vijiji 184 ili kuhakikisha kwamba wananchi wana shiriki kikamilifu katika mradi huo. “Sisi tumejipanga na tutakuwa karibu na ujenzi huu na fursa zote kadiri zitakavyo zinajitoeza tutazitangaza katika tovuti yetu “ na pia watazipata katika halmashauri zao,” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, Bw. James Washima alisema kwamba taasisi yake imejipanga kuwawezesha watanzania kupata uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali na wafanya biashara ili kuweza kuzitumia fursa katika mradi huo mkubwa. “Tunatoa mikopo ya aia mbalimbali tunawakaribisha kuja kuomba mikopo ili wazitumie fursa za mradi huu wa bomba la mafuta,” alisema Bw. Washima. Aliogeza kusema wanaotaka ni vyema kuwa katika vikundi, watapata mikopo wanayotaka ikiwemo ya vitendea kazi na mikopo ya kutekeleza zabuni walizoshida na afuzo ya ujasiriamali. Naye Msajili Msaidizi wa Maendeleo na Tafiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),Bw. David Jere alisema kwamba wakandarasi wanahitajika kujiunga katika ubia ili kuwa na sifa ya kuingia katika mradi huo mkubwa wa ujenzi wa bomba hilo. Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dkt. John Jingu wa pili kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumzia namna baraza litakavyo waelimisha wananchi kutumia fursa za mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania, wa pili kulia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC.
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limejipanga kuanza kutekeleza kwa vitendo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mradi mkubwa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleni Tanga kwa kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi watakaotaka kuzitumia fursa hizo.
Mradi huo mkubwa uliosainiwa mwezi mei mwaka huu na kuwekwa jiwe la msingi hivi karibu na Rais John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda unalenga kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi Beng’i Issa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwisho mwa juma, kwamba wamejipanga kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za ujenzi wa maradi huo kuanzisha shughuli za kiuchumi.
“Tuejipanga vizuri katika kuwaelimisha, kuwaonesha fursa zitakazo kuwepo na kuwapa uwezesha kupitia mifukoa ya uwezeshaji 19,” serikai imeweka fedha katia mifuko hii hivyo waahitajika kuchagamikia,aliongeza kusema Bi. Issa.
Alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutoa fursa za ajira 10,000 na baada ya hapo kutakuwa na ajira 1,000 kwa watanzania, na pia amezitaka Taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA kuendelea kuandaa vijana watakao endana na fursa za ujenzi huo.
Bi. Issa alizitaja shughuli za kiuchumi zinatarajiwa kuwepo katika mradi huo ni biashara za usafirishaji wa bidhaa na watu, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huduma za chakula, uuzaji wa bidhaa za chakula, ulinzi, uuzaji wa vifaa vya ujenzi.
Zingine ni huduma zingine ni kama vile afya, sheria, fedha, bima, huduma za taka, huduma ukarabati na vifaa vya usalama kazini.
Alifafanua kwamba baraza litashirikiana na mikoa ambayo bomba hili linapita kama vile Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na wilaya 24 na vijiji 184 ili kuhakikisha kwamba wananchi wana shiriki kikamilifu katika mradi huo.
“Sisi tumejipanga na tutakuwa karibu na ujenzi huu na fursa zote kadiri zitakavyo zinajitoeza tutazitangaza katika tovuti yetu “ na pia watazipata katika halmashauri zao,” alisema
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, Bw. James Washima alisema kwamba taasisi yake imejipanga kuwawezesha watanzania kupata uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali na wafanya biashara ili kuweza kuzitumia fursa katika mradi huo mkubwa.
“Tunatoa mikopo ya aia mbalimbali tunawakaribisha kuja kuomba mikopo ili wazitumie fursa za mradi huu wa bomba la mafuta,” alisema Bw. Washima.
Aliogeza kusema wanaotaka ni vyema kuwa katika vikundi, watapata mikopo wanayotaka ikiwemo ya vitendea kazi na mikopo ya kutekeleza zabuni walizoshida na afuzo ya ujasiriamali.
Naye Msajili Msaidizi wa Maendeleo na Tafiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),Bw. David Jere alisema kwamba wakandarasi wanahitajika kujiunga katika ubia ili kuwa na sifa ya kuingia katika mradi huo mkubwa wa ujenzi wa bomba hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dkt. John Jingu wa pili kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumzia namna baraza litakavyo waelimisha wananchi kutumia fursa za mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania, wa pili kulia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC. (Picha na Mpigapicha Wetu).
No comments:
Post a Comment