Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa bustani ya kaburi moja iliyopo pembezoni mwa barabara ya Samora wilaya ya ilala kulia kwa Makonda ni Mkuu wa Wilaya ya ilala Sophia Mjema, wa pili (kushoto),ni Mkurugenzi wa JICA Mr. Toshio Nagase hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa bustani ya kaburi moja iliyoko pembezoni mwa barabara ya Samora jijini Dar es Salaam iliyotengwa kwa ajili ya wananchi kupumzika.
Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa jiji la dar es salaam,kutunza na kulinda mazangira ya bustani ya kaburi moja iliyopo maeneo ya samora katika wilaya ya ilala, katika uzinduzi wa bustani hiyo ambayo ilijengwa kwa kiasi cha fedha za kimarekani dola 380,000 lengo la eneo hilo ikiwa ni kwa ajili ya wananchi kupumzika.
Makonda ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa eneo hilo, ambapo Mh. Makonda amekata utepe katika bustani hiyo, ilifanyiwa marekebisho na matengenezo na wadau wa JAICA, wakiwa na lengo la kuijenga dar es salaam mpya, ambayo imeleta muonekano mpya na ni faida kwa wananchi wote watakaotumia sehemu hiyo. Na pia amewataka wafanya biashara wodogo wadogo(wamachinga) kutokufanya biashara katika eneo hilo.
"Eneo letu hili siyo la kufanya biashara kwa ndugu zetu (wamachinga) ni eneo La watanzania wote wanaoitaji kupumzika, tumepajenga ili wananchi wote hatujajenga ili kufanya biashara la hasha! Hili ni eneo la kupumzika kwa mtu yeyote anaehitaji kupumzika baada ya kufanya shughuli zao wengine watapumzika kusubiri magari au mtu anaetaka kujiliwaza anaruhusiwa kupumzika katika bustani hii" Alisema Makonda.
Hata ivyo ameongeza kuwa katika kuboresha maeneo yote ya jiji vituo vya daladala vitafanyiwa marekebisho, ambapo vituo hivyo vikijengwa upya na kuboresha itakuwa ni sehemu nzuri ya kuweka matangazo,na kumjenga jiji hilo na lengo la dar es salaam mpya itatimia.
Pia amesema katika nia ya serikali ya awamu ya tano kubadili dar es salaam kuwa jiji la biashara zidi pamoja na kuhaklikisha mkoa mzima wa Dar es salaamu unakuwa na huduma zote stahiki huku kila mkazi pindi awapo jijini hapo aweze kufurahia matunda ya mkoa na jiji lake pasipo kubudhiwa na mtu yeyote.
No comments:
Post a Comment