Mkurugenzi wa tiba na lishe katika hospital ya Aga Khan akizungumza na waandishi wa habari leo.
Dr Lucy Kwayu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakina mama na watoto waliofika hospitalini hapo.baadhi ya watoto na akina mama waliofika hospitalini hapo ikiwa ni wiki ya unyonyeshaji Duniani.
Hospitali ya Aga Khan imeweka mikakati yake ya Unyonyeshaji ambayo ni maadhimisho dunia nzima yenye lengo kuu la kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama tu katika miezi sita ya mwanzo tokea kuzaliwa kwa mtoto.
Daktari wa watoto na mtaalamu wa lishe na masuala ya unyonyeshaji Dr. Mariam Noorani.
Dr.Mariam Noorani ambaye ni daktari wa watoto na mtaalamu wa masuala ya unyonyeshaji katika hospital hiyo,amesema kuwa katika maadhimisho hayo yaliyoanzishwa na 'The World Allience for Breastfeeding Action' katika mataifa zaidi ya 120,ambapo hospital hiyo ina lengo la kuhanasisha na kutoa elimu ya unyonyeshaji mapema kabla ya mama kujifungua.
Ameongeza kuwa hospital ya Aga Khan ni hospital pekee iliyoidhinishwa kuwa na ubora wa huduma ya unyonyeshaji yenye jina 'Joint Commission' ambayo katika maadhimisho ya mwaka huu hospital hiyo imedhamiria kuhamasisha zoezi la unyonyeshaji wa maziwa na mama kuepuka maziwa ya kopo kwa kuwa hayana faida katika afya ya mtoto.
Aidha Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoadhimisha unyonyeshaji, ambapo waziri wa afya alitangaza mabadiliko katika mazingira ya kazi ili kumwezesha mwanamke kufanikisha kunyonyesha huku akiendelea na kazi, ikiwa ni pamoja na likizo ya miezi mitatu mama apewe miezi mingine sita ya masaa machache kazini ili kumpa wasaa mama kukamua maziwa au kwenda nyumbani kumnyonyesha mtoto.
Pamoja na hayo pia ameongeza kwa kusema kuwa lengo lao ni katika kumuweka mama anaenyonyesha kuelewa ni njia gani itakayo weza kumsaidia katika kukabiliana na changamoto za mama kukosa maziwa ya kutosha kwa mtoto alie chini ya miezi 6 hadi miaka miwili
Na katika kutimiza hayo hospitali hiyo imeandaa sera muhimu Kumi zitakazo mzazi anaenyonyesha kujifunza na kuelewa pia sanjari na hayo wao kama uongozi wa Hospitali ya Aga Khan wamelenga kuanzisha kundi moja la watsupp kwa ajili ya kuwaunganisha wazazi pamoja na wahudumu mbalimbali na kwenye kundi hilo litawasaidia wazazi hao katika kutambua njia mbali mbali za kuwalea watoto,kuwanyonyesha watoto pamoja na kuwasaidia kama watakuwa na uhitaji mbali mbali wa maelezo katika kutambua mambo muhimu yenye kuwa saidia katika kipindi chote cha kunyonyesha.
Katika jambo lingine ambalo imeweza kuwapatia elimu baadhi ya wazazi waliofika kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mbinu mbali mbali zenye kumsaidia mzazi katika sekta nzima ya unyonyeshaji ni pamoja na mzazi mwenyewe kufahamu ya kuwa maziwa ya mama ndiyo yenye umuhimu katika ukuaji wa mtoto hasa kwa kipindi cha awamu ya kwanza ya ukuaji a,mbao ni kati ya miezi 6 ya mwanzo.
Tofauti na kawaida ya baadhi ya wazazi huacha kuwanyonyesha maziwa ya asili na baadae huenda kumpa mtoto maziwa ya unga ambayo yametengenezwa huku akitoa ushauri kuwa maziwa hayo sio mazuri kwa mtoto mchanga na ndio maana wao kama watoa huduma hospitalini hapo mara vnyingi huwa hawapendi kuona biashara ya maziwa ya unga ikifanyika hospitalini hapo labda kwa kibali maalumu tu.
No comments:
Post a Comment