Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel (katikati) akimpongeza mwanariadha Francis Damas leo katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa kupata ushindi wa medali
ya shaba baada ya kushinda mbio za mita 3000 katika mashindano ya
Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko
nchini India.
Katibu Mkuu chama cha Riadha nchini Bw. Filbert Bayi (aliyesimama) akizungumza na
wanariadha na wadau wa mchezo huo mara baada ya timu ya riadha ya
vijana chini ya miaka 17 kurejea nchini na medali ya shaba katika
mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyoalizika hivi karibuni huko chini India.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Bendera ya Tanzania kutoka kwa mwanariadha Regina
Mpigachai mara baada ya kurejea nchini na ushindi wa medali ya shaba
katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya miaka 17 yaliyomalizika
hivi karibuni huko nchini India.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi msaidizi
wa maendeleo ya michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
Mkuu wa Msafara na mwalimu wa wanariadha Bibi Mwinga Mwanjala akitoa neno la shukrani mara baada ya kurejea nchini na ushindi
wa medali ya shaba katika mashindano ya Jumuiya ya madola chini ya
miaka 17 yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.
Timu
ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta heshima kubwa kwa nchi
yetu baada ya kurejea na medali ya shaba aliyoshinda kijana Francis
Damasi katika mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya Jumiya ya Madola
yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.
Timu
hiyo iliyorejea nchini leo imepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ameeleza
kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao ambao
wameitangaza vyema Tanzania.
“Vijana
mmefanya vizuri sana katika mashindano haya Serikali tunawapongeza
sana kwa kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali
ya juu katika mashindano haya nawaahidi kuendelea kushirikiana na
uongozi na wadau wa riadha nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa chama cha riadha nchini Bw. Filbert Bayi
amesema kuwa mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza
Tanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na kushiriki mashindano mengi ya
Kimataifa hivyo ni vyema wadau wakajitokeza kwa wingi kuwekeza katika
mchezo huo ambao umeendelea kuletea heshima Taifa.
“Riadha
imeitangaza Tanzania na itaendelea kuitangaza hivyo wadau wanapaswa
kuona fursa hii na kuwekeza katika mchezo huu ili ufike mbali,kila mtu
katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa ya kizazi hiki na
kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.
Naye
Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo baada kushinda mbio za mita
3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani alijiandaa na
alizingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata ushindi huo
na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza kwani
mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.
Medali
ya shaba katika mahindano ya riadha iliyoletwa na kijana Francis
imerejea tena baada ya miaka 19 tangu Tanzania ilivoshinda medali hiyo
mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment