A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, July 24, 2017

TIMU YA RIADHA YAAHIDI MEDALI LONDON!

Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (mwenye fulana ya bluu) wakati wa ziara ya ofisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John na kulia ni kocha Anthony Mwingereza. Jumla ya wanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
Balozi maalum wa DStv, Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na wanariadha wenzake Nelson Mbuya (wa pili kushoto), Stephano Huche na Joseph Panga(kulia)  wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli.  Wanariadha mbalimbali wameweka kambi jijini Arusha ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya dunia. Jumla ya wanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake Nelson Mbuya (katikati) na Joseph Panga  wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli. 
Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taif ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto) akiwa na Wanariadha wenzake wa timu ya taifa itakayoshiriki Mashindano ya Riadha ya Dunia jijini London wiki ijayo Ezekiel Ng’imba (katikati) na Said Makula wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi  Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London. (PHOTOS: Courtesy of DSTV)

Timu ya Riadha yaahidi Medali London!

BALOZI maalum wa DStv na mmoja wa wanariadha wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia ya mwaka huu yatakayofanyika mwezi ujao jijini London, Uingereza, Alphonce Simbu, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani imejiandaa vizuri.

Akizungumza wakati wa ziara maalum ya Afisa Muandamizi wa DStv, Johnson Mshana katika kambi hiyo iliyopo Ilboru Arusha ambapo pia alishuhudia mazoezi ya timu hiyo, Simbu alisema kuwa yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanaleta medali nyumbani katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika mapema Mwezi Agosti.

“Tumejiandaa vizuri na tuna matumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi mazito na inaonekana vijana tuko sawasawa kupambana katika mashindano hayo” alisema Simbu.

Naye Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Johnson Mshana ambaye alitembelea kambi hiyo na kisha kushiriki katika mazoezi amesema kampuni yao imefurahishwa sana na mwenendo wa kambi hiyo pamoja na timu nzima. “Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi ya timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha haiwezi kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii niyo sababu iliyotusukuma DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya Taifa itakayokwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania washuhudie medali zikija nyumbani”

Amesema baada ya DStv kuanza kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita, wameshuhudia mafanikio makubwa sana. Ambayo yamewatia moyo sana kuamua kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi timu ili hatimaye iweze kufanya vizuri zaidi na kuliwakilisha vyema taifa kwenye michuano ya kimataifa.

“Tulianza na Simbu, amefanya vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi kwa timu yetu ya Tanzania na tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv ilionyesha mbashara Mumbai Marathon tukamuona Simbu akishinda, Tukaonyesha Mbashara London Marathon, tukaona Simbu akivunja rekodi yake, na tutaonyesha mbashara Mashindano ya Dunia Mwezi Agosti, ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua medali kedekede na kuliletea taifa letu sifa kubwa” alisema Mshana kwa kujiamini.

Naye kocha wa timu hiyo, Francis John amesema, kazi kubwa imefanywa na makocha wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kwamba  ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi yao kwenda vizuri. Amesema wanatarajia kuwa wanariadha hao watafanya vizuri  kwani hata mmoja wao aliyekuwa na matatizo ya magoti sasa anaendelea vizuri na bila shaka atashiriki vizuri kwenye mashindano.

Amesema jumla ya wachezaji saba  wakiwemo wanawake watatu na wanaume wanne watashiriki. Failuna Abdi  atashiriki mita 10,000, Gabriel Gerald mita 5,000 na  watano watashiriki marathon kamili ya kilomita 42 ambao ni Magdalena Krispin, Sarah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba na Alphonce Felix Simbu.

Timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo inatarajiwa kuagwa na kukabidhiwa bendera jijini Dar es Salaam tarehe Julai 31 na Mashindano hayo yanaanza tarehe Agosti 4  2017.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages