A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 25, 2017

Chama Cha ADC chamuomba Rais JPM kulegeza masharti ya siasa.



Mwenyekiti wa Chama  Cha Alliance For Democratic Change (ADC), Mdoe Hassan  akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar­-es-salaam Paul Makonda jana walipokwenda kumuomba Rais Dkt.John Magufuli alegeze masharti ya mikutano ya siasa nchini.



Na Yusuph Mlandula



Chama Cha ADC chamuomba Rais JPM kulegeza masharti ya siasa.

Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimemuomba Rais Dkt. John Magufuli kulegeza masharti aliyoyaweka katika siasa ili waweze kufanya mikutano ya hadhara ambayo itasaidia wanachama wao kujua mipango ya chama.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan Doyo mara baada ya kufanya ziara katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Paul Makonda.
Amesema kuwa shughuli za siasa ni haki ya kila chama kikatiba kwani kuzuia shughuli hizo ni kubinya uhuru na taratibu zilizoelekezwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Chama hicvho kinaadhimisha miaka mitano tangu kianzishwe kwa kufanya ziara ya kutemblea vyombo vya habari  mbalimbali ili kuweza kutoa ushirikiano na kujitangaza hasa katika kuelezea mafanikio waliyoyapata.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages