Na Yusuph Mlandula
Viongozi
wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na
uwajibikaji.
Hayo
yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti
wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini
zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.
Askofu
Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika
kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo
imedumu kwa muda mrefu.
“Lukuvi
ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais
John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua
kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.
Ameeleza
kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri
kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu
matumizi ya ardhi na umuhimu wake.
Askofu
Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya
ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona
kuwa ni mali.
Mhe.
Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo
limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao,
aliongeza Askofu Mwamalanga.
Kiongozi
huyo wa Dini amesema kuwa Mhe. Lukuvi ni mfano wa kuigwa na mawaziri na
viongozi wenzake kwa uchapakazi wake. Amesema kuwa ni Waziri ambaye
anawashirikisha watendaji waliochini yake katika maamuzi mbali mbali,
hivyo anastahili kupewa tuzo.
“Tumepanga
kumpa tuzo Waziri Lukuvi kwa kuzingatia yafuatayo: Kuiweka ardhi
mikononi mwa watanzania, kuonyesha kuwa ardhi ni chanzo kikuu cha uchumi
wa watu na utatuzi wa migogoro ya ardhi hasa iliyodumu kwa muda mrefu”,
alisema Askofu Mwamalanga.
Migogoro
hiyo ni kama vile mgogoro wa kijiji cha Mabwegere, Mkoani Morogoro,
mgogoro wa Chasimba, jijini Dar es Salaam na migogoro mingine mingi
katika mikoa ya Arusha, Mbeya, Kigoma, Tanga na Mwanza.
Askofu
Mwamalanga amesema Kamati yake imewasiliana na Taasisi mbalimbali za
Serikali na binafsi ili watoe mapendekezo ya tuzo ambayo anastahili
kupewa Mhe. Lukuvi kwa utendaji kazi wake mzuri.
Amezitaja
baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni Vyuo Vikuu vya Umma na Binafsi, Marais
wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu, Vyama vyote vya siasa ambavyo kwa
ujumla wake vimeonyesha kutambua mchango wa waziri Lukuvi.
Baada
ya kupokea mapendekezo na kuyafanyia kazi ndipo itatangazwa siku ya
kutoa tuzo hiyo kwa Mhe. Lukuvi, alisema Askofu Mwamalanga.
Tangu Waziri Lukuvi aiongoze Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mwisho mwa uongozi wa awamu ya Nne hadi sasa,
mabadiliko
yenye tija katika wizara hiyo yameonekana. Migogoro mingi ya ardhi
imetatuliwa, utoaji wa hati za viwanja umerahisishwa na huduma kwa
wateja imeboreshwa.
No comments:
Post a Comment