A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 5, 2017

DC SOPHIA MJEMA APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHUO CHA ST.MARK KATIKA KUELIMISHA JAMII

DC SOPHIA MJEMA APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHUO CHA ST.MARK KATIKA KUELIMISHA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.
Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akianza ziara kukagua maeneo mbalimbali yanayokizunguuka chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Mark Dr.Peter Kopweh akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya alipokuwa akizuru maeneo mbalimbali katika chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji Ilala Bw. Benjamin Chagula wakati akiangalia namna ya kutatua Changamoto ya mipaka ya chuo hicho inaingiliwa na wananchi wanaoishi eneo jirani.
 
Na Yusuph Mlandula

Nae katika hotuba yake Mh.Mjema ambaye alipata fursa ya kuzungukia maeneo kadhaa chuoni hapo alieleza lengo kuu la kufika chuoni hapo kadhalika kupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zinazofanyika.

“Nimeamua kutoka na kuja kuwaona kwani nauthamini sana uwepo wenu katika wilaya yangu (Ilala) kwani hii ni fursa muhimu ya serikali kuwatumia wasomi hata waliopo vyuoni kutatua Changamoto katika maeneo waliyopo, mimi nakazia hapa wilayani na naamini ujio huu utakuwa wenye tija sana kwetu sisi pamoja nanyi kama taasisi katika kushirikiana” alisema Mh. Sophia Mjema.

Kadhalika akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho, Mh.Mjema alitangza kufungua milango ya fursa kwa wasomi hao kufika ofisini kwake na kuleta mawazo pamoja na nguvu zao ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele huku akikazia suala la uzalendo pamoja na wito wa Mh Rais Magufuli kuhusu kufanya kazi.

Vilevile Mh. Mjema alikazia suala la kuimarisha misingi ya elimu ya juu kwa kuwekeza kwenye uboreshaji wa teknolojia kwani dunia ya sasa mitandao umekuwa nyenzo muhimu ya kupata taarifa za kitaaluma.

“Mkakati wa kusambaza huduma ya intaneti (WIFI) katika vyuo vikuu hapa Ilala unaendelea kwa kasi na umesimama kwa muda kutokana na hali ya mvua lakini baada ya hali hii kila kitu kitakuwa kama ilivyoahidiwa,lazima msome kisasa” alihitimisha.

Nae Rais wa chuo kwa niaba ya wanafunzi wote alifikisha Changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la mikopo pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwani limekuwa likidhohofisha maendeleo ya taaluma alitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya na kuahidi ushirikiano na ofisi ya wilaya pamoja na kujitoa kutumia taaluma zao ndani ya jamii kwa ujumla.

Akihitimisha zoezi hili pamoja na kumshukuru Mh.Mjema kwa kufika chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Chuo hicho hasa wakati huu ambapo milango ipo wazi kwa wanafunzi kudahiliwa vyuoni moja kwa moja huku akiwaondoa hofu wale wanaobanwa na kazi kuwa watapata fursa ya kusoma masomo ya jioni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages