Mkuu
wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza na
waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka
Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC (hawapo pichani) kuhusu
malengo ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za
fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and
Reporting System (FFARS).
Baadhi
ya Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara
Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati
alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa
uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama
Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
Baadhi
ya Waratibu wa Elimu Kata kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara
DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani
Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya
siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji
taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial
Accounting and Reporting System (FFARS).
Sehemu
ya Waratibu wa Elimu Kata na Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka
Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje
(hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna
ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha
unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and
Reporting System (FFARS).
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje
(aliyekaakatikati) akiwa pamoja na baadhi ya waratibu wa elimu kata
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mara baada ya ufunguzi wa mafunzo
ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji
taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial
Accounting and Reporting System (FFARS). Aliyeketi kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa
Waganga
wafawidhi wa vituo vya afya, na Waratibu elimu kata kutoka Halmashauri
93 zilizo katika mikoa 13 nchini inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini wameanza mafunzo ya siku mbili juu
ya namna ya kutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha
unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and
Reporting System (FFARS).
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa,
mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya
kutolea huduma na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu
ya mapato na matumizi ya halmashauri.
Bwana
Wengaa alisema kuwa kuunda kwa mfumo huo kutasaidia kuhakikisha fedha za
ruzuku zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa
usahihi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.Alisema kuwa FFARS itawapatia watoa
huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa
za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyao.
Bwana
Wengaa aliongeza kuwa FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo
katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na
sheria za manunuzi na utoaji taarifa. “Taarifa hizi zitasaidia Serikali
kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na
hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia,”
alisema.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yanafanyika katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara
inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
ambapo waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya
wanashiriki.Aliitaja mikoa hiyo 13 kuwa ni pamoja na Mtwara, Lindi,
Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mara,
Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Kigoma, na Kagera.
Mafunzo
hayo yanafanyika katika ngazi ya halmashauri, ambapo mjini Mtwara
mafunzo hayo yaliwahusisha waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na
Waratibu elimu kata kutoka Halmashauri za Manispaa ya Mtwara Mikindani
na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Akifungua
mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani
Bibi Beatrice Dominick, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi
Sambwe Sijabaje alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma wa
vituo vya halmashauri hizo mbili kuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa
za mapato na matumizi, na hivyo kuchangia uwajibikaji na utoaji wa
huduma bora kwa wananchi.
Alisema
kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa mfumo wa kielektroniki ili kuendana na
wakati na mabadiliko ya teknolojia na mfumo wwa kujaza vitabu
ulioboreshwa ili kukidhi changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwemo
umeme na kukosekana kwa huduma ya mtandao wa intaneti kwa baadhi ya
vituo vya kutolea huduma.
Hata
hivyo baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Halmashauri za Manispaa
ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wameiomba
Serikali kuwapatia vitendea kazi kama vile Laptop ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi uliokusudiwa.
Mfumo
huo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais –
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na
Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.
Mafunzo
hayo yanatarajiwa kuwanufaisha Waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na
Waratibu elimu kata kutoka zaidi ya Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800,
Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule za Msingi na Sekondari
20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment