Upo
usemi wa wahenga usemao “mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.” Hivi
ndivyo ninavyoweza kusema kuhusiana na harakati za Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika
kuhakikisha kuwa Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi inaimarika.
Dkt.
John Pombe Magufuli kabla ya kuteuliwa kuwa Rais, amekuwa Waziri katika
Awamu mbili zilizopita. Anao uzoefu mkubwa wa utendaji kazi lakini pia
katika kuongoza Wizara ambapo amewahi kuwa Waziri wa Ujenzi na
Miundombinu na Kilimo na Ufugaji.
Kutokana
na umuhimu wa Sekta ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi katika maendeleo
ya Taifa, mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais, aliagiza ujenzi wa
barabara ya kutoka Mwenge hadi Moroco ambayo ilikuwa ina msongamano
mkubwa wa magari kuelekea katikati ya jiji.
Msongamano
huo umekuwa ukiathiri malengo ya Wafanyakazi ambao walikuwa wakitumia
muda mwingi wakiwa kwenye foleni na hivyo kupunguza muda wa kufanya kazi
lakini pia uzalishaji na utoaji huduma za msingi kwa Taifa.
Aidha,
Mheshimiwa Rais ameshiriki uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa
ujenzi wa barabara za juu (fly over) katika makutano ya barabara ya
Nyerere na Mandela eneo la Tazara unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni
100 za Kitanzania na pia ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya
barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es
Salaam
Hivi
karibuni Serikali kupitia Waziri Mwenye dhamana ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi
ambacho kimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya M/S Songoro Marine
Transport Boatyard ya Mwanza.
Kivuko
hicho kilichogharimu jumla ya Shilingi bilioni 7.3 za Kitanzania, ni
moja ya ahadi ya Mheshimiwa Rais John Magufuli alizozitoa wakati wa
Kampeni zake za Urais za kuwapunguzia kero za usafiri Wananchi wakiwemo
wakazi wa Kigamboni.
Akipokea
Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 Prof.
Mbarawa amesema lengo la Serikali ni kuboresha huduma za kusafirisha
abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni ambapo kwa muda mrefu
kimekuwa kilio cha Wananchi waishio kigamboni.
Kabla
ya ujio wa kivuko hicho kipya kumekuwa na jitihada zizolikuwa zinafanywa
na Serikali katika kutatua tatizo la usafiri kwa Wananchi wa Kigamboni
kwa njia ya Pantoni.
Moja
ya jitihada katika kukabiliana na tatizo hilo ni ujenzi wa Kivuko cha MV
Magogoni chenye uwezo wa kubeba abiria 2000 na magari 60 kwa pamoja
sawa na Tani 500.
Profesa
Mbarawa amesema Kivuko cha MV Kazi kinakwenda kuimarisha usafiri kwa
Wakazi wa Kigamboni ambapo kwa sasa kutakuwa na jumla ya Vivuko vitatu
kikiwemo pia kivuko cha…..
Aidha,
uzinduzi wa daraja la Kigamboni ni moja ya mafanikio makubwa ambayo
yanafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayotekeleza Ilani yake ya
Chama Tawala cha CCM.
Daraja
hilo licha ya kuunganisha wananchi wa Kigamboni lakini pia
linaunganisha watu wote ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo nchini hasa
kwa wakazi wa Kigamboni.
Daraja
la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 linaunganisha upande wa Kurasini
na Kigamboni wenye urefu wa Kilometa 2.5. Ujenzi wa daraja hilo
umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na Kampuni
ya China Bridge Engineering Group na umegharimu zaidi ya shilingi
bilioni 250 za Kitanzania.
Kwa
maoini yangu, utendaji wa jinsi hii unatoa taswira ya uwajibikaji
mahsusi unaopaswa kufanywa na viongozi wa Kisiasa ukihusisha usimamizi
na ufuatiliaji yakinifu wa Sera/michakato/mikakati na mipango ya
serikali.
Usimamizi
na ufuatiliaji unaofanywa na Prof. Mbarawa uwe chachu kwa Viongozi
wengine wa Serikali na Wanasiasa waliopewa dhamana katika awamu ya Tano.
Si jambo geni kumsikia Prof. Mbalawa kwa siku moja akiwa katika mikoa
miwili tofauti akifuatilia utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya
Tano.
Wapo
watu wanaoweza kubeza uwajibikaji wa Waziri huyu lakini kimsingi
anachofanya ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata huduma ya msingi
katika kuwaletea maendeleo yao na Taifa kwa jumla. Ndio maana nimesema
kuwa “mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.”
No comments:
Post a Comment