
MBUNGE
wa Mafinga Mjini,Mh. Cosato Chumi sambamba na mwenyekiti wa halmashauri ya
mji wa mafinga Charles Makoga wakikata utepe wa kuzindua gari la kubebea
wangonjwa (AMBULANCE) la kituocha afya cha Igohole
hawa
ni baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari
hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato
Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto
MBUNGE
wa Mafinga Mjini, Mh. Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la
kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha
Igohole ya wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake
hilo.
Gari
hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa uongozi wa
halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho
katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.
Akikabidhi
msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo
limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto. Uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane
vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la
Mafinga.”
Alisema
gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa
lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa
hospitalini.
Baada
ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo
jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake
kuwa ni kuhakikisha jimbo la mafinga mjini linapata huduma bora ya maji,
elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Akishukuru
kwa msaada huo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk
Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, kituo hicho cha afya
kilikuwa hakina gari hata moja la kubeba wagonjwa.
“Pamoja
na kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya, kurikuwa na magari mawaili tu
ambayo yalikuwakihudumia vituo vingine 18 vya kutolea huduma katika
wilaya hiyo hivyo,” alisema Mhagama.
Alisema
kupatikana kwa gari hilo jipya kutasaidia kuboresha huduma hiyo kwa
kuokoa maisha ya wagonjwa na maisha ya mama na mtoto ambayo ni
kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya.
Akizungumzia
huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo ya wilaya, Dk Mhagama
alisema kwa wastani wajawazito 500 wanajifunga kila mwezi hospitalini
hapo.
“Kati
yao wajawazito zaidi ya 100 huwa wanapata huduma za dharula huku wastani
wa wajawazito 10 wakipatiwa huduma za rufaa,” alisema dr Mhagama.
Naye
mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Charles Makoga alisema
halmashauri yake kwa kushirikiana na mbunge huyo itahakikisha
inatekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa na Chama cha Mapinduzi (CCM),
Rais Dk John Magufuli, mbunge na madiwani ili kuboresha huduma kwa watu
wake.
No comments:
Post a Comment