Shirika la Save the
Children nchini limeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kukutana na
Watoto mbalimbali wa shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya
Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo Walimu na
Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii walishiriki na kuchangia
mijadala iliyoibuliwa na watoto wenyewe kuhusu malengo ya usawa na haki
ya jinsia ifukapo mwaka 2030.
Katika tukio hilo baadhi ya shughuli
walizofanya watoto ni pamoja na kuibua mijadala ya Haki na Wajibu wa
Mtoto, Unyanyasaji na changamoto za kurepoti kesi za unyanyasaji. Watoto
walipata majibu jinsi ya kuripoti kesi za ukatili na unyanyasaji katika
kituo cha dawati la jinsia kwenye kituo cha Polisi karibu nao.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni, Bi. Halili Katani wakati wa kufungua mjadala wa
Siku ya Mtoto wa Afrika, alieleza kuwa, Watoto wana haki na wajibu wa
kusaidiwa pamoja na kulindwa kama wajibu wa Serikali na Jamii yote.
Alitoa wito na rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa, haki za watoto
zinatimizwa na kulindwa na kuwafikia watoto zikiwemo za elimu, ulinzi
na malezi bora.
Aidha, aliwataka watoto hao wakawe mabalozi
wazuri wa kutoa elimu kwa wenzao kwa kuwapa elimu waliopata katika siku
ya Mtoto wa Afrika.
Bi Halili aliwataka watoto Manispaa ya
Kinondoni na maeneo mengine kuhakikisha wanaripoti matendo ya kikatili
pindi watakapofanyiwa huko mitaani ama na walezi wao kwa kutoa taarifa
kwa watu wanaowaamini ikiwemo Walimu, Maafisa wa Ustawi wa jamii na
madawati ya Jinsia katika ngazi mbalimbali ikiwemo kwenye Kata, Vituo
vya Polisi na sehemu zingine.
Naye Meneja wa Mradi wa Elimu ya Afya ya
Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru amesema kuwa,
watoto wenyewe wamebaini kutokuwa na usawa katika malezi yao huku
wakilalamika kuwa wamekosa upendo kutoka kwa wazazi / walezi kutokana na
aina ya maisha ya baadhi ya familia.
“Shughuli hii ni maalum kwa watoto wa
Manispaa ya Kinondoni ambapo watoto wenyewe pamoja na walimu wao
wameweza kuelezea hali halisi wanayopambana nayo huko majumbani na
mashuleni hivyo changamoto hizo zimepokelewa na walimu wenyewe pamoja na
maafisa Maendeleo ya Jamii hatua zaidi ya utekelezaji zimewekwa bayana
hapa.” Alieleza Bi. Ellen.
Aidha, amewasihi wazazi kuwa na desturi ya
kufuatilia watoto wao hasa mienendo ya maisha na makuzi yao kwani watoto
wamekuwa na maisha mabaya katika makuzi yao.
Shughuli zingine kwenye tukio hilo ni pamoja
na watoto hao kuonyesha igizo maalum, mijadala ya wazi ya wao kwa wao
pamoja na kuamsha mijadala ya kujifunza kutoka kwa maafisa wengine
waliokwemo.
Kwa mwaka huu Siku ya Mtoto wa Afrika
Kitaifa inatarajia kufanyika hapo kesho Juni 16.2017, Mkoani Dodoma huku
ikiwa na kauli mbiu “Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto”.
Katika maadhimisho hayo, Jumla ya
shule 10 za Manispaa hiyo ya Kinondoni ziliweza kushiriki huku baadhi
ya shule hizo ni pamoja na : Mbezi Ndumbwi, Salasala, Mikocheni A,
Ushindi, Mikocheni B Sekondari, Nakasangwe, Changanyikeni, Makongo Juu
na nyinginezo.
Meneja wa Mradi wa
Elimu ya Afya ya Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru
akitoa elimu katika tukio hilo la siku ya Mtoto wa Afrika 2017, ambapo
maadhimisho hayo yamefanyika mapema leo Juni 15, Manispaa ya Kinondoni
Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mratibu wa Ulinzi kwa Watoto wa
Save The Children, Bi. Haika Harrison.
Baadhi ya watoto waliokuwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Manispaa ya Kinondoni jana Juni 15.2017.
Mratibu wa Ulinzi kwa Watoto wa Save The Children, Bi. Haika Harrison akiwaimbisha watoto nyimbo mbalimbali
Watoto hao wakitoa burudani
Afisa wa Save the Children kutoka Sweden- Award Manager, SCS, Bwana. Olle Kvist akizungumza na watoto hao katika ghafla hiyo.
Afisa wa Save the Children kutoka Sweden- Award Manager, SCS, Bwana. Olle Kvist akizungumza na watotokatika ghafla hiyo
Afisa mipango wa Save the Children, Mzee John Komba 'JK' Kijana akizungumza jambo katika ghafla hiyo
Baadhi ya walimu wakifuatilia tukio hilo
Baadhi ya watoto wakitoa maelezo namna ya michoro yao katika mradi maalum wa watoto katika baadhi ya shule unaoendeshwa na Save the Children
No comments:
Post a Comment