Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Na Yusuph Mlandula
Chama
Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za
uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa
kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha,
kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.
Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa
wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia
Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola
vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
HAMPHREY POLEPOLE, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais MAGUFULI
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia
raslimali za Taifa.
POLEPOLE amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais
MAGUFULI hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya
Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi
wa nchi.
Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema kilichofanywa na Rais
MAGUFULI ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza
kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya
Madini hapa nchini.
Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na Mmliki wa
Kampuni ya Barrick Gold Cooparation kwa kukiri kukosea na kuahaidi
kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa
mara watakachokubaliana baada ya mazungumzo na Tanzania.
No comments:
Post a Comment