A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 15, 2017

Maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani Yafana Muhimbili


 Mkuu wa Wilaya yaIlala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema akizungumza na Jonas Hans Atile (kushoto) ambaye amejitokeza kuchangia Damu katika wiki yakuchangia damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Praxeda Ogweyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani. Pia Dk. Ogweyo amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu jana jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Wananchi akishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu duniani Leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH jana.
 Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchangia damu Leo katika jengo la Maabara kuu, hospitali ya Taifa Muhimbili jana.
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Muhimbili wakiendelea na shughuli ya utoaji damu jana.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki katika madhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu duniani kwa kuendesha shughuli ya utoaji damu kwa watu mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wenye uhitaji.


Shughuli hiyo inaendelea katika hospitali hiyo kwenye Jengo la Maabara kuu ambako watu wamekusanyika kwa ajili ya kuchangia damu. Mmoja wa viongozi walishriki katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema pamoja na Watanzania mbalimbali.


Akizungumza katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wakiwamo kinamama na watoto wadogo.


“Nawapongeza wote walifika leo hapa Hospitali ya Muhimbili kuchangia damu, ni jambo la muhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema Mheshimiwa Mjema.


Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa hospitali hiyo, Dk Praxeda Ogweyo amewataka wananchi,mashirika  ya umma na yasiyo ya kiserikali, shule, vyuo mbalimbali na taasisi za dini  kujitokeza kuchangia damu hospitali hapo.


Dk Ogweyo amesema kuwa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100 hadi 120 kwa siku na kwamba damu inayokusanywa ni kati ya chupa 50 hadi 60 na upungufu wa damu ni chupa 60 hadi  hadi 70, hivyo damu inahitajika zaidi.


“Kutokana na hali hii, naomba rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuokoa maisha ya wagonjwa. Hospitali imejipanga kupitia kitengo chake cha uchangiaji damu kilichopo maabara kuu hivyo karibuni mchangie damu,” amesema Dk Ogweyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages