Na Yusuph Mlandula.
Wakati
kipenga cha ufunguzi wa kigi kikipigwa agosti 20 mwaka 2016 kwa mchezo
wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga ilikua ni kitu kilichokua
kikisubiliwa na wapenzi wengi kutokana na wadau kushuhudia usajili
kabambe wa vilabu vyao.
Kuanza
kwa ligi kuliweza kutoa harufu ya msisimko na ushindani katika msimu
huo,mfano mechi ya kwanza kati ya Azam Fc dhidi ya African Lyon ilikua
mechi ambayo iliwaduwaza sana mashabiki na benchi la ufundi la azam
kutokana na shughuli waliyokutana nayo toka kwa vijana wa African lyon.
Azam
katika mchezo huo ilisawazisha dakika za mwisho baada ya Lyon
kutangulia kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja na kumshinda kipa
Aishi manula.
Kwa
upande wa ratiba wadau wengi ambao wengi wao ni wanazi wa simba na
yanga walilalamikia kwa kuona timu moja wapo ina pendelewa.
Changamoto
ya ratiba imekua ni mfupa ulioshindikana kabisa kutokana ligi kusimama
Mara kwa Mara au kutoa viporo kwa baadhi ya timu kutokana na kuwajibika
kimataifa .
Mapendekezo
yanayoweza kuwa bora ni uandaaji wa ratiba wa ligi kuu utazame kalenda
ya FIFA pamoja na ile ya CAF ili wanapopanga wasiweze kuleta
mkanganganyiko na kusababisha viporo.
Kwa
upande wa usajili uliozua zengwe na kuleta mkanganyiko ni ule wa
mchezaji Said mkopi aliyekuja kufungiwa baada ya Tanzania Prisons
kupeleka pingamizi na kuonekana mkopi ana mkataba na klabu yake ya
zamani huku akisajiliwa tena Mbeya City.
Maamuzi
yalitotokea kwa Mkopi yalishindwa kutokea kwa mmoja wa Wachezaji wa
African Lyon ambaye akikatiwa rufaa na klabu ya Yanga baada ya kuonekana
alikua na pingamizi toka moja klabu ya ligi kuu nchini na mwisho wa
siku TFF ilishindwa kufanya maamuzi hayo kwa wakati baada ya uchunguzi
ilikuja kumfungia mchezaji huyo lakini pendekezo la klabu ya Yanga
kupata point Tatu kutokana na mchezo huo haikufanyika.
Zengwe lingine ilikua ni usajili wa Hassan Ramadhan Kessy kutoka klabu ya Simba na kusaini klabu ya Yanga.
Picha
la kessy lilianza kuwekwa wazi katika fainali ya FA msimu wa 2015/2016
iliyoikutanisha Azam fc na Yanga baada ya mchezo Kessy alijitokeza
katika jezi ya yanga huku akilakiwa vyema na Mpinzani wake wa nafasi
Juma Abdul Jaffary Mnyamani.
Mizengwe
iliendelea kwani Tangu mwanzo wa msimu viongozi wa tff wakijikuta ktk
wakati mgumu kwa kuwaondoa Geita Gold mine Fc na kuwapa nafasi Mbao Fc
ambayo haikutarajia kucheza ligi kuu msimu uliomalizika.
Moja
ya mambo ya kiufundi waliyokuwa wameiyafanya vilabu vya simba yanga na
Azam yalikua na tija kwa vilabu hivyo kwani yalileta matokeo chanya
mfano maamuzi ya azam kuachana na wahispania wale kulileta matokeo
mazuri na kufanya klabu kufikia hatua ya NNE kwani kama wangeendelea
kubaki na Wahispania wale kungeiangusha vibaya zaidi klabu ya Azam.
Kwa
upande wa klabu ya simba maamuzi ya kumpa mkataba omog kulikua na faida
kubwa kama ilivyokua kwa yanga kumbadilisha Mwalimu kulileta matokeo
chanya pia.
Miongoni
kwa kanuni zilizoshangaza wadau wengi ni lile sakata la kadi tatu za
Novatus Lufunga na kadi tatu za Mohammed Fakhi zilizoleta mkanganyiko
mkubwa na kukiuka taratibu za Mpira duniani.
Waweza kusema linaloshindikana Ulaya Tanzania linawezekana na watu wakalifungia Kazi na kuaminisha umma kuwa ni halali.
Kwa
upande timua timua ya wachezaji hakuna mdau aliyetegemea golikipa wa
Simba Vincent agban kama angekumbana na fagio la kuondoka klabuni au
Jean Baptista Mugiraneza wa azam ambao walionekana kuwa ni wachezaji
nguli kama ilivyokua kwa mbuyu twite wa yanga aliyempisha Justin Zulu.
Tabia
ya mchezaji toka timu ndogo akiisumbua timu kubwa wakikutana ni kama
anajipigia kampeni ya kusajiliwa imezidi kudhihirika kwani klabu ya
yanga walifanya usajili wa Emmanuel Martin toka JKU ya Zanzibar kwa
mtindo huo ,pia mchezaji Pastory Atanas mchezaji wa zamani wa stand utd
alisajiliwa Simba baada ya kuifunga klabu ya yanga .
Uhamisho
kwa upande wa Wachezaji wageni ilikua gumzo kwani ilikuja kuonekana
kwamba klabu yeyote toka nje ya Tanzania iliyopata kuonyesha uwezo wake
hapa nchini kulifanya vilabu kuwafuatilia na kuwasajili wachezaji hao.
Hii ni moja ya Tabia za kitanzania ambapo viongozi wetu hawana muda wa
kufuatilia wachezaji nje ila wanasubiri waje nchini ndipo wawaone hii
inatoa maana kuwa hatuna uwezo mzuri wa kufuatilia wachezaji huko huko
nje.
Azam na simba waligawana wachezaji wa Medeama ya Ghana Mara tu walipowaona wakikabiliana na Yanga hapa nchini.
Klabu
ya mbao nikitegemea ingekuwa ndo klabu bora na hata kocha wao
ingewezekana angekuwa kocha bora kutokana na mazingira waliyokua nayo
mbao fc,moja ya sifa ambayo walikua nayo ni kutengeneza chemistry nzuri
kuanzia eneo la mlinda mlango hadi ushambuliaji.
Ingeweza
kusemwa kuondolewa kwa Kipa wa mbao Erick Ngwegwe kungeweza kuiathiri
timu lakini mbadala wa ngwegwe ambaye ni Benedict Haule a.k.a Berko
kuliwashangaza wengi na akamaliza msimu vyema.
Yako
mambo ambayo vilabu vya majeshi vinaweza kujitathimini na kutazama ni
mtindo upi wautumie katika kuwa na timu ligi kuu, wangeweza kuwa na
klabu moja na kuitunza vyema na mishahara mizuri na kuweka falsafa ya
kusajili hadi nje ya nchi katika kuimarisha vilabu vyao .
Simaanishi
wachezaji wa ndani sio wazuri hapana ila najaribu kutazama namna
watakavyo weza kubadili mifumo na kuwa vilabu vya kupambana kwaajili ya
mataji na sio kufanya mchezo kwao ni kama ziada.
Nini kifanyike.
Pendekezo
lililotolewa na uongozi yaani bodi ya ligi kwa kuhitaji maoni katika
mapendekezo ya marekebisho ya kanuni ni moja ya kitu kizuri sana ambacho
kitaweza kupunguza au kama sio kuondoa kabisa mikanganyiko
inayojitokeza.
Kamati
inayohusika na hadhi ya wachezaji wanatakiwa kufanya Kazi kwa weredi
bila kusukumwa na upande wowote au mihemko ya watu Fulani.
Wachezaji
ni bora wakajitambua na kuachana na uhuni wa kizamani ambao mwisho
unakuja kukugharimu hili nalisema kutokana na lile lililomkuta Saidi
Mkopi ambaye kajikuta anakaa nje kwa kutokucheza kabisa msimu mzima.
Klabu
zijenge utamaduni wa kufanya mazungumzo na Klabu zingine pale
inapofikia hatua kutaka kumchezaji toka klabu nyingine na kuachana na
tabia ya kuzungumza na mchezaji ambaye mwisho wa siku klabu inaingia
hasara ya kulipa faini kwa usajili wa kificho.
Yako
mambo mengi ya kiswahili ambayo kamati ya ligi inapaswa kuyachunguza
vyema hasa Yale ya klabu kutoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Ulinzi
ulio bora kwa kutumia askari na sio mabaunsa katika vyumba ndio
suluhisho la malalamiko ya vyumba kupuliziwa dawa kama madai yao
yalivyo.
Kwa
upande wa msisimko wa mashabiki uko juu sana na klabu vimekua vikitoa
ushindani mkubwa,ni nadra kuona simba anashinda mchezo wa mbao kirahisi
Kazi kubwa inafanyika mchezo wa yanga dhidi ya ndanda unakua na msisimko
na usio kuwa na matokeo ya moja kwa moja hii inatufanya tuamini kuwa
mpira wetu unapambana kutaka kuifanya ligi yetu na msisimko mkubwa.
Kila
idara katika uongozi ikifanya vyema inatoa matokeo chanya vilevile hata
vilabu vikiwa na viongozi wenye kusimamia kanuni toka shirikisho navyo
vita kuwa na nidhamu na haitatokea mambo ya vilabu kuruka ukuta au
kugomea zawadi.
No comments:
Post a Comment