A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, June 7, 2017

ACT WAZALENDO WAKUTANA LEO KUTAFAKARI UTEUZI WA MWENYEKITI WAO WA CHAMA KUTEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA MOSHI




Kamati ya uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo inatarajia  kukutana leo juni 7 kutafakari namna ambayo mwenyekiti wao wa chama Anna Mghwira ambavyo atatekeleza wajibu wake katika chama hicho na majukumu mapya aliyoyapata.

Akitoa taarifa hiyo Katibu wa itifaki na Uenezi na mawasiliano ya umma wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema chama hicho kimepokea taarifa kuhusu uteuzi wa mwenyekiti wao wa chama  hicho kuwa mkuu wa   mkoa wa Kilimanjaro.

"Taarifa za Mwenyekiti wa chama chetu kuwa mkuu wa mkoa wa kilimanjaro uteuzi usika umefanyika wakati mama Mghwira akiwa nje ya nchi na baada ya kurejea amefanya mazungumzo na viongozi wenzake wa juu wa chama kuhusu uteuzi wake" alisema Shaibu.

Chama hicho kimewataka wanachama wake kuwa na utulivu wakati wa vikao vya chama vinavyochukua hatua stahiki kuhusu jambo hilo.

 June 3, 2017 Rais Magufuli alimteua Mwenyekiti wa Taifa Chama cha ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages