A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 31, 2017

Tanga Cement yakabidhi msaada wa jengo la darasa na choo wilayani Mkinga, Tanga

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Samuel Shoo (wa pili kulia), akishikana mikono wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kichalikani, Robert Kimario  wakati akikabidhi msaada wa jengo la darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Mkinga mkoani Tanga jana. Kulia ni Ofisa Masoko na Mawasiliano wa TCPLC,  Hellen Maleko na wa pili kushoto ni Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mkinga,  Zakayo MlInduka. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Samuel Shoo (wa nne kulia), akishikana mikono na Kaimu Mkurungezi Mtendaji Wilaya ya Mkinga, Michael Ndunguru wakati akikabidhi msaada wa darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Mkinga mkoani Tanga jana. Wanaoangalia ni baadhi wanafunzi wa shule hiyo. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo. 
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Hellen Maleko  akishikana mikono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kichalikani, Robert Kimario (wa pili kulia), wakati akikabidhi msaada wa jengo la darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Mkinga mkoani Tanga jana. Wa tatu kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Samuel Shoo. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo. 
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Hellen Maleko  akishikana mikono na Ofisa Elimu Wilaya ya Mkinga, Zakayo Mlenduka (wa tatu kushoto), wakati akikabidhi msaada wa jengo la darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Mkinga mkoani Tanga jana. Wa tatu kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Samuel Shoo. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imetumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo.
Msimamizi wa Fedha  wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Ahmed Mhadi, akishikana mikono na Mwenyekiti  wa Kijiji cha Kichalikani, Khalfani Ally (kushoto) katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa jengo darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika shuleni hapo, Mkinga mkoani  Tanga jana. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR)  imetumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo. Kushoto kwa msimamizi huyo wa fedha ni Ofisa Masoko na Mawasiliano, Hellen Maleko na Meneja Mauzo, Samuel Shoo.
Mtaalamu wa Tehama   wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC),Coleman Mbando, akishikana mikono na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kichalikani, Halima Hulifani (wa tatu kushoto),  walipokwenda kukabidhi msaada wa darasa lililojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya makabidhinao ilifanyika eneo  la shule, Mkinga mkoani Tanga jana. Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR) imeshatumia kiasi cha shs milioni 44.9 kukamilisha ujenzi wa darasa hilo pamoja na choo.  wengine ni baadhi ya wafanyakazi Tanga Cement na wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages