A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, November 10, 2026

TANAPA YATANGAZA MAFANIKIO MAKUBWA YA UTALII NA UHIFADHI TANZANIA 2026

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeeleza mafanikio makubwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, likiwa limeongeza idadi ya watalii kutoka 700,000 mwaka wa fedha 2021/22 hadi zaidi ya milioni 1.5 mwaka 2025/26, huku mapato yakiongezeka kutoka shilingi bilioni 174 hadi zaidi ya bilioni 534 katika kipindi hicho.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari leo Novemba 10, 2026, jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana Gibril Mwishawa, amesema idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 24, hatua inayoonesha ukuaji wa shughuli za utalii katika hifadhi za taifa.

Amesema sambamba na ongezeko la watalii, makusanyo ya shirika yamepanda kutoka shilingi bilioni 174 mwaka 2021/22 hadi zaidi ya shilingi bilioni 534 mwaka 2025/26, jambo linaloongeza uwezo wa shirika kuendeleza shughuli za uhifadhi na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwishawa amesema katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, TANAPA imejipanga kutekeleza miradi yote ya maendeleo iliyopangwa pamoja na kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta ya utalii, hatua inayotarajiwa kupanua fursa za kiuchumi na kuongeza ajira kwa vijana katika mnyororo mzima wa thamani wa utalii, ikiwemo usafiri, malazi, huduma za chakula na shughuli nyingine zinazohusiana na sekta hiyo.

Amesisitiza kuwa mafanikio ya uhifadhi hayapaswi kuangaliwa kwa wingi wa wanyamapori, misitu na maliasili nyingine zinazolindwa pekee, bali pia kwa namna shughuli za uhifadhi zinavyoboresha maisha ya wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi na jamii kwa ujumla.

“Mafanikio ya uhifadhi hayawezi kupimwa kwa maliasili tunazozihifadhi pekee, bali yatapimwa pia kwa maisha ya wananchi kutokana na uhifadhi tunaoufanya,” amesema Mwishawa.

Kauli hiyo inaweka msisitizo katika umuhimu wa kuunganisha uhifadhi na maendeleo ya wananchi, ili ukuaji wa sekta ya utalii uende sambamba na upatikanaji wa fursa za ajira, uwekezaji na manufaa ya kiuchumi kwa jamii, huku rasilimali za taifa zikiendelea kulindwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages