A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 30, 2026

BENKI YA ABSA YAENDELEA KUJIZATITI KATIKA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI NCHINI

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Victor Nchimbi akizungumza na baadhi ya wajasiriamali kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo hususani zinazowalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati, katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani ambayo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudhamini tukio hilo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hili liliwakutanisha zaidi ya wajasiriamali 350, viongozi wa sekta, na watunga sera chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kushirikiana katika kuendeleza ukuaji wa biashara zinazochochea injini ya uchumi wa taifa.

KATIKA kutambua mchango wa wanawake wajasiriamali katika kuinua Uchumi wa Taifa, Benki ya Absa Tanzania imeendelea kuhamasisha wajasiriamali hao kujiunga na akaunti ya SHE ya benki hiyo ambayo pamoja na faida nyingine, akaunti hiyo haina makato ya mwezi ya kuendesha akaunti, ada za kufanyia miamala na kuweza kufanya miamala kwa kutumia fedha za kitanzania na za kigeni.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ambayo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudhamini, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo, Bw. Victor Nchimbi alisema kwa kupitia akaunti ya SHE, wanajasiriamali wanawake wanapata mafunzo maalumu ya jinsi ya kuendesha biashara zao kwa mafanikio.

Tukiwa kama wadau wakubwa wa sekta hii ya ujasiriamali na kwa kutambua mchango wa wajasiamali Tanzania tumekuwa na huduma mbalimbali tunazowapatia wajasiriamli wetu, ikiwa ni pamoja na mikopo yenye gharama nafuu, huduma za kidigitali, ukiangalia katika maadhimisho haya, waadhimishaji wengi ni wanawake, tunayo akaunti ya SHE, iliyojikita katika kuwawezesha wanawake kuichumi”, alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, mmoja wa wajasiriamali anayejishughulisha na biashara ya vipodozi, Bi. Maua Jumanne alisema, suala la elimu ya mitaji, mikopo na jinsi ya kufanya biashara kwa ufanisi limekuwa ni changamoto kwa wanawake wajasiriamali wengi, hivyo akatoa ushauri kwa benki mbalimbali kuyapa uzito mambo hayo.

Natoa ushauri kwa watu wa mabenki kutufikia na kutupa elimu ya mitaji na mikopo ya kutusaidia sisi wajasiriamali wadogo tuweze kukua katika biashara zetu, na kuepukana na mikopo inayotolewa na vikundi vya watoa mikopo vya kausha damu”, alisema Bi. Maua.

Benki ya Absa imeendelea kujitolea katika kuunda majukwaa yanayofikika kwa urahisi ambapo Biashara Ndogo, Ndogo za Kati na za Kati, zinaweza kubadilishana mbinu bora za biashara, kupata fursa za ufadhili, na kuhamasisha ubunifu, huku ikidumisha lengo kuu la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya jingine'.
Meneja Bidhaa wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Devroda Kagusa (kulia) akizungumza kuhusu huduma zizotolewa na benki hiyo hususani zinazowalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati, kwa baadhi ya wahudhuriaji waliofika katika banda lao, katika Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani ambayo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudhamini, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hili liliwakutanisha zaidi ya wajasiriamali 350, viongozi wa sekta, na watunga sera chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kushirikiana katika kuendeleza ukuaji wa biashara zinazochochea injini ya uchumi wa taifa.
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Absa, Bi. Mboni Sabura (katikati) akizungumza na baadhi ya wajasiriamali kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo hususani akaunti maalumu ya wanawake ya She, katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani ambayo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudhamini, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kulia ni Meneja Bidhaa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Devroda Kagusa. Tukio hili liliwakutanisha zaidi ya wajasiriamali 350, viongozi wa sekta, na watunga sera chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kushirikiana katika kuendeleza ukuaji wa biashara zinazochochea injini ya uchumi wa taifa.
Meneja Bidhaa wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Devroda Kagusa (kulia) akizungumza kuhusu huduma zizotolewa na benki hiyo hususani zinazowalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati, kwa baadhi ya wajasiriamali waliofika katika Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani, ambayo Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kuwezesha tukio hilo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hili liliwakutanisha zaidi ya wajasiriamali 350, viongozi wa sekta, na watunga sera chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kushirikiana katika kuendeleza ukuaji wa biashara zinazochochea injini ya uchumi wa taifa.
Baadhi ya wawezeshaji na wajasiriamali waliojitoleza kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wajasiriamali Duniani wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kukamilika kwa tukio hilo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Benki ya Absa ilikuwa moja ya taasisi zilizojitokeza kudhamini hafla hiyo. Tukio hili liliwakutanisha zaidi ya wajasiriamali 350, viongozi wa sekta, na watunga sera chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ili kushirikiana katika kuendeleza ukuaji wa biashara zinazochochea injini ya uchumi wa taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages