A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 18, 2026

MBUNGE WA SEGEREA AWAKUMBUKA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM.

 

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Agnesta Lambert (CHAUMA), ameendeleza juhudi zake za kuimarisha ustawi wa makundi maalum kwa kuwafikia watoto wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Msingi ya Viziwi Buguruni, jijini Dar es Salaam ambapo amekabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji mengine muhimu, kwa lengo la kuwawezesha watoto hao kusherehekea kwa heshima na furaha sikukuu za Idd el-Fitr na Pasaka.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge huyo ameeleza kuwa anahisi kuwajibika kusimamia masuala ya kijamii, hususan yanayohusu watoto wenye mahitaji maalum na kusisitiza kuwa uwekezaji katika ustawi na elimu ya watoto hao ni msingi muhimu wa kujenga jamii jumuishi na yenye usawa wa fursa.

‎Amebaini changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo, ni upungufu wa mabweni kwa wanafunzi hao na kuahidi kufikisha suala hilo bungeni na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu, na hivyo ana imani kuwa changamoto zilizopo zitapatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo ameeleza kuwa uhaba wa mabweni unawaweka watoto hao katika hatari, ikiwemo uwezekano wa kupata ajali kutokana na mazingira yasiyo rafiki kwa hali yao.

‎Wanafunzi hao wakatoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum, wakisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kijamii katika kujenga mustakabali bora kwa wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages