Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Maruma (Katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja naye ni watendaji waandamizi wa benki hiyo.
BANK Of Africa Tanzania, (BOA)imeungana na sehemu nyingine duniani katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024, chini ya kauli mbiu “Above and Beyond” na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na wigo mpana kuhakikisha tunafikia malengo makubwa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki wa huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji, Esther Maruma amesema wateja katika benki hiyo wanapewa kipaumbele kikubwa katika kila mipango wanayofanya.
"Tunaamini kuwa huduma bora kwa wateja siyo tu kuwapatia huduma za kifedha bali ni pamoja na kujenga uhusiano mzuri na wa muda mrefu baina yetu na wateja hivyo wiki hii ya Huduma kwa Wateja 2024 ni fursa ya kutambua na kusherehekea imani ya wateja wetu kwetu pia tukithamini kujitoa kwa wafanyakazi wetu wanaofanya kazi bila kuchoka kutoa huduma bora". Amesema Esther.
Katika kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa karibu zaidi na wateja wake alisema, Bank of Africa Tanzania karibuni ilianzisha huduma ya “BOA Wakala” inayowezesha wateja kuweka na kutoa fedha bila kulazimika kutembelea matawi yake na kuboresha zaidi huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (B-Mobile) ili iweze kutumiwa na wateja kwa urahisi na kwendana na matakwa yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa Bank of Africa, Annaroberta Mango, amesema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wafanyakazi wa Benki watapata fursa ya kuongea na wateja kwenye matawi, kupokea maoni yao sambamba na kuwapatia ushauri wa kifedha katika kuimarisha biashara zao.
“Tunajivunia timu yetu ya Wafanyakazi yenye moyo wa kujitolea kufanikisha kutoa huduma bora kwa wateja wetu kila siku. Wiki hii pia ni nafasi yetu ya kutambua mchango wao mkubw... ni matarajio yetu tutaisherekea pamoja na wateja wetu na kuwashukuru kwa kuichagua Bank of Africa na kuwadhihirishia jinsi tunavyowathamini kwa kuendelea kutuamini". Amesema Mango.
Nae Conrad Leo, mmoja wa wateja wa Benki hiyo amesema amekuwa mteja kwa kipindi cha miaka mitano katika benki hiyo na anafurahia na kuridhika na huduma zinazotolewa kwani hata anapokuwa na changamoto za kibiashara amekuwa akipatiwa suluhisho.
Katika wiki ya Huduma kwa Wateja Benki itakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoshirikisha wafanyakazi na wateja ikiwemo kuwashukuru wateja, kuwazawadia wafanyakazi,mafunzo zaidi kwa wafanyakazi kutoa huduma kwa wateja na kushiriki huduma za kijamii na kutoa msaada kwa jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akiwa na watendaji waandamizi wa benki hiyo kwenye picha ya pamoja katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Maruma (kushoto) akikata keki pamoja na mmoja ya wateja wa benki hiyo, Bw Conrad leo (Katikati) kwenye sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja , kulia ni Wasia Mushi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ) wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Maruma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Maruma wa pili kushoto akitoa zawadi kwa mmoja ya wateja wa benki hiyo, Conrad le, mwanzo kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ), Wasia Mushi na mwanzo kushoto ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Annaroberta Mango.
No comments:
Post a Comment