Na Chalila Kibuda,Dodoma
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na teknolojia ya mashine ya kutengeneza udongo wa Udongo wa kuoteshea mazao ya bustani ikiwemo mbogamboga.
Akizungumza katika Banda la VETA katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma Afisa Ufuatiliaji na Tathimini ya Mafunzo VETA Mhandisi Joseph Kimako amesema teknolojia itasaidia mkulima kuwa na uhakika WA kuota mazao aliyopanda bila kuwepo kwa mimea mingine.
Amesema kuwa udongo unaotengenezwa unaondolewa magugu ili kuhakikisha mimea inayopandwa unaota wenyewe pasipo Kuota mmea usiohitajika.
Kimako amesema wakati wa uandaji vitalu unaweka mbegu za nyanya wakati wa uotaji unaota na na mbegu nyingine ambayo haijakusudiwa inaota Jambo ambalo kwa Kutumia Udongo huo mmea unaota uliokusudiwa.
Hata hivyo amesema Udongo kama huo unatoka nje ya Nchi,VETA imetengeneza mtambo huo ili kiwasidia wakulima waweze kupata Udongo kwa kwa Bei rasihi ambao unatengenezwa kwa Kutumia malighafi za ndani.
Aidha amesema Teknolojia hiyo ni rafiki kwa mkulima katika kuendesha Kilimo cha kisasa na uhakika baada ya kutumia udongo huo.
Katika Maonesho hayo wakulima watumie fursa ya kupita Banda la VETA kujifunza Teknolojia hiyo.
No comments:
Post a Comment