Mwenyekiti wa Taasisi ya Mazingira na Maliasili Tanzania Mwanawetu Saidi akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari hawapo pichani
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
TASISI isiyo ya kiserikali ambayo inajihusisha na utunzaji wa mazingira Mkoani Pwani inayofahamika kama Mazingira na Utalii nayoongozwa na Mwanawetu Saidi wamefanya ziara katika shule za Muheza na Mount Calvary.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mwanawetu amesema kuwa wametembelea Shuleni hapo ili kutoa elimu ya kuhifadhi na kutunza mazingira kwa faida ya vizazi vijavyo.
"Tunasisitiza jamii kujiunga na klabu za kutunza na kulinda mazingira sambamba na kutumia nishati safi" amesema Mwanawetu.
Amesema kuwa Taasisi yao inajihusisha na kutoa elimu kwa jamii katika kutunza mazinga ya baharini na nchi kavu ikiwemo wanyama wa porini kwa ujumla.
Wakiwa Shuleni hapo wamesisitiza matumizi ya nishati safi katika kupika chakula cha wanafunzi na kuacha kutumia mkaa na kuni.
Muasisi wa Partnership for Green Future Rehema Peter amesema kuwa jukumu lao kubwa ni kutoa elimu ya utunzaji mazingira na safari yao imeanza kwa kutembelea Shule ya msingi Muheza,Kibaha ambapo wamekuta kuna chagamoto za ukosefu wa matundu ya choo tunaendele kutafuta wadau ili shule zetu za msingi ziwe na mazingira safi na salama.
"Tusitumie kuni wala mkaa katika kumuunga mkono Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi.
Akizungumza kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mount Calvary Eric Kilonzo amesema wamefurahishwa na ugeni wa wanamazingira hao na wamepokea hamasa ya utunzaji mazingira na wameanza mchakato wa kuandaa majiko ambayo yatapika kwa kutumia nishati safi.
No comments:
Post a Comment