A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 31, 2023

KAMPUNI YA UBER YATANGAZA DONGE NONO KWA WATEJA WAKE WATAKAOFANYA MALIPO KWA TIGOPESA

Meneja wa kampuni ya Uber ukanda wa afrika mashariki Imran Manji (wapili kushoto), akishika na mikono na Afisa Mkuu wa Kampuni ya Tigo Kitengo cha TIGOPESA Angelica Pesha (wapilikulia), wakiashiria uzinduzi rasmi wa  kampeni  ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakao tumia Uber na Tigopesa wengine kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Uber  Monica Mziray pamoja na Afisa kutoka kampuni ya tigo. Hafla Hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Mkuu wa Kampuni ya Tigo Kitengo cha TIGOPESA Angelica Pesha akizungumza wakati wa hafla ya ya kutangaza ubia wakufanya kazi pamoja na kampuni ya Uber Tanzania  kwa muda wa mwaka mmoja wa kampeni  ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakaotumia Uber na Tigopesa .



Meneja Uendeshaji wa Uber  Monica Mziray akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza ubia wakufanya kazi pamoja  na kampuni ya tigo kwa muda wa mwaka mmoja wa kampeni  ya kutoa zawadi kwa madereva na wasafiri watakaotumia Uber na Tigopesa .

 

Kuanzia sasa, madereva wanaotumia mfumo wa Uber wanaweza kujisajili kama wakala wa Lipa kwa Simu ya Tigo Pesa, ambayo itawawezesha kupokea nauli kutoka kwa wasafiri watakaopenda kulipa nauli zao kupitia mitandao ya simu.

 Madereva wanaotumia mfumo wa Uber wataweza kupata pesa zao kutoka kwenye akaunti za Lipa kwa Simu bila makato yoyote kutoka kwenye mawakala wa Tigo Pesa kwa kiasi chochote chini ya Tshs. 500,000 kwa siku.Abiria watakaotumia huduma ya Lipa kwa Simu ya Tigo pesa watarudishiwa 10% ya nauili watakayolipa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa, sambamba na kampeni hii, Uber itaendelea kufanya kampeni zingine kupitia app yao.

 Madereva watakaotumia huduma ya Lipa kwa Simu kwa malipo yao ya nauli watarudishiwa 20% ya ada ya malipo kwa kila muamala unaofanywa kupitia Lipa Kwa Simu.Meneja wa Uber Afrika Mashariki, Bw Imran Manji anasema, “Tuna furaha kubwa kuingia Ubia na kampuni ya Tigo katika kufanikisha kampeni hii itakayowasaidia madereva kuongeza kipato, na pia abiria kuokoa pesa kila wanapotumia mfumo wa Uber.

Ubia huu ni muhimu na una tija kubwa kwa sababu inawafanyia wepesi abiria na madereva kufanya miamala wanapotumia mtandao Uber, ikiwa ni pamoja na wateja ambao hawana akaunti za benki na wamepungukiwa na pesa taslimu.”Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Pesa, Bi. Angelica Pesha amesema: “Ubia huu tunaoingia na kampuni ya Uber unaonesha waziwazi nia ya Tigo Pesa kufanikisha malengo yake ya kusambaza huduma za kifedha katika jamii ya Watanzania.

 Sasa madereva wa Uber watapata huduma watapata huduma ya malipo ambayo inahakikishia abiria wao njia salama na rahisi ya kulipa nauli wanaposafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Sambamba na hilii, ubia huu ni ushahidi kwamba huduma ya Lipa Kwa Simu ni huduma yenye ufanisi mkubwa na tunategemea kwamba huduma hii itasaidia biashara ndogondogo kuendele kukua.

”Sekta ya usafiri wa teksi za mitandaoni imeleta mageuzi makubwa katika namna ambayo tunasafiri katika miji yetu, na tangu walipofungua milango yao jijini Dar es Salaam mwaka 2016, Uber amekuwa mshirika mkubwa wa jiji hilli kupitia huduma za usafiri, kuchangia katika uchumi kwa kutoa fura za kiuchumi sambamba na kuchangia katika mapato ya serikali.

Imran anahitimisha kwa kusema, “Tuna matumaini makubwa na soko ka Tanzania na kunzishwa kwa programu kama hizi zitachochea ukuaji wa biashara, sambamba na kuimarisha ubora wa huduma kwa abiria.”

Kuhusu Uber Dhamira ya Uber ni kuwasaidia watu kutumia simu ili kupata usafiri - kila mtu na mahali popote. Tulianza mwaka 2009 kwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo dogo: unawezaje kutumia simu yako kuita usafiri? Baada ya kufanya zaidi ya safari bilioni 10, tumeanza kutafuta ufumbuzi wa tatizo kubwa zaidi: kupunguza foleni ya magari na uchafuzi wa mazingira katika miji mbalimbali kwa kutumia magari machache kusafirisha watu wengi Uber inatoa huduma zake katika miji zaidi ya 60 Kusini mwa Jangwa la Sahara

 (Cape Town, Durban, Joburg, Pretoria, Gqeberha (zamani ikijulikana kama Port Elizabeth), East London, Polokwane, Cape West Coast, Worcester, Emalahleni / Middelburg, Garden Route, Rustenburg, Potchefstroom, Mbombela (zamani ikijulikana kama Nelspruit), Newcastle, Mthatha, Thohoyandou, Upington, Margate, Richards Bay, Welkom, Phuthaditjhaba, Ermelo, Queenstown, Nairobi, Mombasa, Nakuru, Ibadan, Warri, Owerri and Akure Enugu, Kano, Port Harcourt, Lagos, Abuja, Benin City, Abidjan, Kampala, Accra, Kumasi, Tamale na Sunyani).

 Kwa ujumla, huduma za Uber zinapatikana katika miji zaidi ya 10 000 katika nchi 65. Ili msafiri aweze kuita gari To request a ride, users must download the free application for Android, iPhone, Blackberry 7, or register for Uber at www.uber.com/go.

  Uber inatoa huduma zake katika miji kumi na tatu Kusini mwa Jangwa la Sahara (Cape Town, Durban, Joburg, Pretoria, Port Elizabeth, Nairobi, Mombasa, Lagos, Abuja, Kampala, Accra, Kumasi and Dar es Salaam). Kwa jumla mtandao wa Uber unapatikana katika miji zaidi ya 600 na zaidi ya nchi 65. Ili msafiri aweze kuita gari, ni lazima aweke app ya Uber ya simu za Android, iPhone, Blackberry 7, au ajiandikishe kutumia Uber kupitiawww.uber.com/go. Kwa maswali tafadhali tembeleawww.uber.com

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages