A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 18, 2023

MCHEZAJI WA SIMBA SC SAKHO AITWA KUITUMIKIA TIMUYAKE YA TAIFA

 Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Pape Ousmane Sakho amejumuishwa kwenye Kikosi cha Wachezaji 24 wa timu ya taifa ya Senegal (Simba wa Terenga) ambacho kitacheza michezo ya kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofanyika nchini Ivory Coast mwaka 2023.

Sakho ambaye anacheza kwenye Klabu hiyo ya soka ya Tanzania, safari hii ameaminiwa na Kocha wa timu hiyo ya taifa, Aliou Cisse ambaye ndiye aliyechagua Wachezaji hao watakaounda Kikosi hicho kitakachocheza (back to back) dhidi ya timu ya taifa ya Msumbiji, katika Kundi L la kuwania kufuzu Michuano hiyo ya AFCON.

Kiwango cha Sakho katika Klabu ya Simba huenda kikawa kimemvutia Kocha Cisse kumjumuisha kwenye Kikosi cha timu ya taifa.

 Sakho amewahi kushinda tuzo ya Goli bora la mwaka barani Afrika, 2022 akifunga bao hilo kwa mtindo wa ‘Acrobatic Kick’ dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sakho alifunga bao hilo kwa mtindo wa ‘Acrobatic Kick’ kwenye dakika ya 12 ya mchezo baada ya kupokea Pasi safi ya ‘krosi’ kutoka upande wa kulia wa Shomari Kapombe, bao hilo lilikuwa la kwanza kwa Simba SC kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Asec kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Hata hivyo, Kocha Aliou Cisse sanjari na Mshambuliaji mahiri wa timu hiyo ya Senegal anayecheza Bayern Munich ya Ujerumani, Sadio Mane walikutaka na Sakho kwenye tafrija ya kutoa tuzo hizo mbalimbali iliyofanyika mjini Rabat, Morocco, Julai 21, 2022.

Kwenye Kikosi hicho cha Simba wa Teranga (Senegal), wapo Magolikipa, Alfred Gomis, Seny Dieng na Mory Diaw.

Walinzi ni Kalidou Koulibaly, Youssouf Sabaly, Noah Fadiga, Moussa Niakhate, Abdoulaye Seck, Abdallah Ndour, Ismail Jakobs na Farmose Mendy.

Viungo ni Idris Gana Gueye, Nampalys Mendy, Krepin Diatta, Pape Gueye, Pape Matar Sarr, Pathe Ciss, Dion Lopy.

Washambuliaji ni Sadio Mane, Habib Diallo, Baoulaye Dia, Bamba Dieng, Pape Ousmane Sakho na Iliman Ndiaye.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages