A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 18, 2023

INFANTINO MINNE TENA FIFA

 Na Mwandishi Wetu


Rais wa shirikisho la Soka Duniani Gianni Infantino amesema ataendelea kuimarisha  sekta ya soka ulimwenguni kwa kuinua kiwango cha mpira wa Miguu kwa  watoto wadogo. 



Infantino ameyasema hayo mjini Kigali Rwanda baada ya kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miaka minne ijayo kuliongoza Shirikisho hilo la Soka Ulimwengu.


Gianni Infantino alichaguliwa kwa wingi wa kura za wajumbe wote 208 waliohudhuria kongamano la 73 la FIFA lililofanyika Kigali kati ya nchi 211 wanachama wa FIFA.


Kongamano la FIFA mjinpi Kigali lilianza mapema wiki hii ambapo zilifanyika shughuli kadhaa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Kigali uliopewa jina la Pele nyota wa Brazil aliyengáa kwenye medani za soka ulimwenguni’


Mara baada ya kuchaguliwa tena Gianni Infantino amesema atazidisha ushirikiano wa mataifa wanachama wote wa Shirikisho.


“Nawahakikishia kuendeleza ushirikiano wa pamoja nanyi,, napenda niwakumbushe kwamba michezo ni starehe, furaha, mapenzi na amani." Amesema 


Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba wakati ambapo dunia inatawaliwa na siasa za chuki, soka ni kiunganishi muhimu. Mataifa yanapaswa  kushirikiana ili kukomesha tabia mbaya ya ubaguzi


“Mashabiki wanapowarushia ndizi mbivu wachezaji wa kiafrika, hii ni kwa sababu ya mazingira mabovu ya kijamii ambayo yanasababisha tabia hizo mbovu.Kwa hiyo tunatakiwa kushirikiana kuhakikisha kwamba michezo inakuwa jumuishi na ya kuheshimiana” amesema Kagame.


Naye nyota wa zamani wa Nigeria Jay Jay Okocha amesema maandalizi ya kongamano la 73 la FIFA na mafanikio yake ni ishara kwamba sasa Afrika inaanza kujizatiti zaidi


“Hili ni jambo ambalo waafrika wote tunapaswa kulichukulia kama letu na ni ishara kwamba kumbe tukiweka nguvu zetu pamoja tunaweza kufanikiwa” amesema Okocha.


Kwenye kongamano hilo Gianni Infantino (52) amesifiwa kutokana na mafanikio yake katika kuleta mabadiliko katika ufanisi wa maendeleo ya mashirikisho ya mpira katika mataifa wanachama wa FIFA.


Ruzuku ya pesa kwa mashirikisho ya mpira ilipanda kutoka dola laki mbili na nusu hadi milioni mbili ndani ya kipindi cha miaka saba iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages