A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, October 6, 2022

Wafanyakazi Benki Ya Exim Wasafisha Magari Ya Wateja, Wagawa Zawadi Wiki Ya Huduma Kwa Wateja

 Benki ya Exim Tanzania hii leo imeungana na watoa huduma ulimwenguni kote kusherehekea wiki ya Huduma kwa Wateja huku ikiahidi kuendelea kuwa karibu zaidi na wateja wake kupitia huduma zenye ubunifu zaidi kwenye soko la huduma za kifedha.


Katika kuthibitisha kauli hiyo maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Jaffari Matundu walishuhudiwa wakiwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kufanya matukio mbalimbali kwa ajili ya wateja ikiwemo kusafisha magari ya wateja mbalimbali waliofika kupata huduma kwenye tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

Akitoa salamu za heri kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi hilo Bw Matundu alisema pamoja na jitihada za benki hiyo kuvutia wateja wapya kupitia huduma mbalimbali za kisasa zinazoeandana na mahitaji ya wateja hao, benki hiyo pia imekuwa ikiweka msisitizo mkubwa katika kuwahudumia wateja wake waliopo.

"Wiki ya Huduma kwa Wateja imetoa tena nafasi nzuri kwa benki kusherehekea jukumu muhimu ambalo tumekuwa tukilifanya kila siku yaani kuwahudumia wateja wetu na kuonyesha umuhimu wa ushirikiano baina yetu kama uongozi, wafanyakazi pamoja na wateja wetu,’’ alisema.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu Idara ya Fedha, Shani Kinswaga alipongeza wafanyakazi wote wa benki hiyo akisema utoaji bora wa huduma ni kiungo muhimu katika kuhakikisha wateja hao wanaridhika huku akiwataja wafanyakazi hao kama mashujaa muhimu ambao wamekuwa wakihakikisha wateja wanaridhika kupitia huduma bora wanazozitoa.

"Zaidi pia ningependa tuendelee kuzingatia na kujitolea katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu ambao wameendelea kuwa waaminifu kwetu pia.” alisema Kinswaga wakati akihimiza timu ya wafanyakazi hao kujisikia fahari kwa michango yao.

Katika maadhimisho hayo, mbali na zoezi la uoshwaji wa magari ya wateja ilishuhudiwa wakuu wa Idara mbambali wa benki hiyo wakiwahudumia kifungua kinywa wateja mbalimbali waliofika kwenye baadhi ya matawi ya benki hiyo sambamba na kujadili pamoja maswala muhimu ikiwemo namna bora ya uboreshaji wa huduma za benki hiyo pamoja na kujadili fursa zinazopatikana kupitia ukuaji wa biashara.

Huku akisisitiza kuwa kila siku ni siku ya huduma kwa wateja katika benki hiyo, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro alisema benki imeendelea kujitolea kutoa kiwango cha huduma zenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wake na wadau bila kujali hali zao au wapi walipo kote nchini.

"Kama sehemu ya hatua za kurejesha fadhila na uaminifu wa wateja wetu, wiki hii yote tumekuwa na shughuli kadhaa za kipekee na maalum kuonyesha namna tunavyowathamini wateja. Baadhi ya shughuli ni pamoja na kutembelea wateja kwa kushtukiza na kuwazawadia kama njia ya kuwashukuru kwa kuwa waaminifu kwetu.,’’ alisema

Wakizungumzia mapokezi hayo pamoja huduma za benki hiyo baadhi ya wateja wa benki hiyo Bw Hamisi Kozzy kutoka Kampuni ya Business Index pamoja na Bw Rashmit Lathigara kutoka kampuni ya Vin Mart waliipongeza benki hiyo kwa huduma zake za kisasa na zinazoendana na mahitaji yao.

"Kuridhika kwetu na huduma zinazotolewa na Benki ya Exim ndiko kunatufanya tuendelee kupata huduma zetu kupitia benki hii. Ni matumaini yetu kwao kwamba ari hii haitapungua na tupo tayari kupokea mambo mazuri zaidi kutoka kwao,’’ alisema Bw Kozzy.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (Kulia) akiwaongoza maofisa waandamizi wa benki hiyo kusafisha magari ya wateja wa benki hiyo waliofika kupata huduma kwenye tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni mmoja wateja wa benki hiyo Bw Bw Rashmit Lathigara kutoka kampuni ya Vin Mart.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (wa tano kulia) na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiwa tayari kusafisha magari ya wateja wa benki hiyo waliofika kupata huduma kwenye tawi la makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (kulia) akifurahia pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.



Wafanyakazi wa Benki ya Exim, wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Frank Matoro wakikabidhi keki kama ishara kuwatakia heri na mafanikio wateja mbalimbali wa benki hiyo wakati wakanyakazi hao waliwapomtembelea wateja hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam leo.












No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages