A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 9, 2022

MAENDELEO BANK YASHEREHEKEA MIAKA 9 TANGU KUANZISHWA KWAKE

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka 9 toka kuanzishwa kwa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba akizungumza wakati wa hafla ya kusherehekea miaka 9 toka kuanzishwa kwa benki hiyo. Wenginepicha ni ma Afisa wa Maendeleo benki pamoja na wachungaji wa makanisa ya KKKT Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba (kushoto), Pamoja na Mchungaji Mkuu wa Jimbo la kati Frank Kimambo (katikati) ambae pia amemuakilisha Askofu Mkuu wakikata keki kuashiria uzinduzi rasmi ya sherehe za kutimiza miaka 9 toka kuanzishwa kwa Maendeleo Benki, ambapo leo kutafanyika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu salama unaofnyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mkuu wa Jimbo la kati Frank Kimambo akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr. Ibrahim Mwangalaba wakati wa sherehe ya kufurahia miaka 9 ya Maendeleo Bank wengine ni wachungaji wa Makanisa ya KKKT.
Wafanya kazi wa Maendeleo Bank wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kusherehekea miaka 9 ya Benki hiyo.

Imeelezwa kuwa ongezeko la wateja zaidi ya elfu 60 katika kipindi cha miaka tisa kwa benki ya maendeleo nchini kumeifanya benki hiyo kufikisha mali za thamani ya shilingi bilioni 102 huku ikifikisha amana ya shilingi bilioni 72 hali inayo ifanya benki huyo kuwa mbioni kuingia katika benki za kitaifa


Akizungumza leo jijini Dare slaamu  katika hafala ya kutimiza miaka 9 ya benki ya maendeleo mkurugenzi mtendaji wa benii ya maendeleo nchini ibrahim mungalaba amesema benki hiyo imeendelea kukua kimtaji na wateja huku katika kipindi cha miaka tisa imechangia shilingi bilioni 10 kama kodi kwa serikali huku ikitoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 200.


Ameongeza Mkurugenzi kuwa maendeleo bank  katika kipindi cha nusu ya mwaka benki hiyo imepata faida ya zaidi ya shilingi milioni 754 huku wakitarajia ongezeko la mara mbili kufikia mwisho wa mwaka na hivyo kuifanya kutoa gawio  kubwa kwa wana hisa.


Pia amewataka watanzania na wateja wa benki ya maendeleo waendelee kuitumia benki hiyo kwani wamejipanga kuboresha huduma zake na kutanua wigo ili kuhakikisha maendeleo benki inamfikia kila mmoja ndani ya Tanzania.


Kwa upande wake mwakilishi wa askofu wa Dayosisi ya mashariki na pwani ambao ndio waanzilishi wa benki hiyo frank kimambo ameeleza kuwa mipango ya baadae ni kutanua wigo wa huduma matawi ya benki hiyo ili kutoa nafasi kwa watazania kuhudumiwa na benki hiyo popote walipo  kutoka matawi  machache yaliyopo sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages