A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 27, 2022

ELIMU SACCOS LTD YAUPIGA MWINGI,YATOA MAFUNZO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI KWA WANACHAMA WAKE.

 CHAMA Cha Kuweka na Kukopa Elimu Saccos Ltd Morogoro, kimeendelea kutanua wigo baada ya kutoa Mafunzo ya elimu ya biashara na Ujasiriamali kwa Wanachama wake.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Juni 25/2022 katika Ukumbi wa Bwalo JKT lililopo Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mwenyekiti wa Elimu Saccos Ltd ,Herman Njerekela ambaye ndiye aliyefungua mafunzo hayo, amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Wanachama wake waweze kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato mara wanapo chukua mikopo.

Njerekela, amesema kumekuwa na changamoto kubwa hususani katika kuzalisha fedha za mikopo kwa baadhi ya Wanachama wa Saccos.

Aidha, amesema kuwa mara baada ya Mafunzo hayo Wanachama watakuwa na uwaledi mkubwa wa kuanzisha biashara zao pamoja na usimamizi mzuri wa fedha.

" Tumeona tuwe na Semina ya Mafunzo elekezi kwa Wanachama wetu, tumekuwa tukitoa mikopo mingi lakini elimu ya kuitumia hiyo mikopo imekuwa changamoto, kupitia Mafunzo haya Wanachama wetu watakopa fedha na kuanzisha biashara wakiwa na uhakika mkubwa wa marejesho ya fedha" Amesema Njerekela.

Hata hivyo, Njerekela, amesema wameokoa jumla ya zaidi  Milioni 60 ambazo ni madeni ya Wanachama huku akitoa wito kwa Wanachama kurejesha fedha Kwa wakati ili kulinda uhai wa Chama.

Mwisho, ametoa rai kwa Wanachama kuwa Chama hakitamvumilia mwanachama yeyote atakaye daiwa hivyo kuwataka warejeshe badala ya kuanza kufuatiliana na kuchukua hatua ambazo wamekuwa wakizitumia kupitia makato ya hadhina.

Naye Afisa Ushirika akimwakilisha Mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro, Jedida Jerry ,  amewataka Wanachama kusikiliza kwa makini Mafunzo hayo ili kupata uzoefu wa kuwa na elmu ya biashara katika kukuza fedha zao wanazo kopa.

Kwa upande wa mtoa Mafunzo, Alfred Mwanyika, amesema Mafunzo hayo Kama watayazingatia basi wataweza kukuza mitaji yao na kujiendesha katika kufikia malengo yao.

Miongoni mwa Wanachama, Zenna Lutego ,amesema amefurahishwa na Mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi huku akiwataka Wanachama wenzake kujikita katika uzalishaji.

Mbali na hapo, Elimu Saccos Ltd ,imezindua Website yake kwa ajili ya kutoa habari mbalimbali pamoja na matangazo yanayohusu Chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages