WIZARA ya Afya inampango wa
kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 20 kati 1000 kufikia vizazi
hai 15 kati ya 1000 ifikapo mwaka 2025 huku ikiweka mkakati pia wa
kupunguza visa vya watoto waliozaliwa wafu kutoka 16 kati ya 1,000
kufikia visa 12 kati 1,000 ifikapo mwaka huo.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu
Mkurugenzi kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Catherine
Sungura amesema huduma za afya kwa watu wote zinahitajika katika ngazi
zote ikiwa ni Zahanati kila Kijiji, Kituo cha Afya kila Kata na
Hospitali kila Wilaya.
Kuhusu vifo vya watoto amesema Wizara
inampango wa kupunguza vifo vya Watoto chini ya miaka 5 kutoka 50 kati
1,000 hadi kufikia Watoto 38 kati 1,000 ifikapo 2025.
Wakati
katika mimba za Utotoni Wizara inampango wa Kupunguza mimba za utotoni
kwa wasichana walio na umri kati ya 15 hadi 19 toka asilimia 27 ya sasa
kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2025.
Akizungumzia Mkakati wa
Pamoja wa Huduma za Mama na Mtoto No. 3 Sungura amesema kwamba Wizara
ya afya inampango wa Kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka 250
kati100,000 kwa sasa kufika 100 kati ya 100,000 ifikapo 2025.
"Kupunguza
visa vya maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa
kujifungua kutoka 8% kufikia 2% ifikapo 2025." Amesema Catherine.
Amesema
kuwa Wizara inavipaumbele vya Kuboresha Huduma, Matibabu, Dawa na
Huduma kwa Mteja ili kukidhi mahitaji yanahihitajika na Mgonjwa ama
mteja.
Aidha amesema wizara inafanya maboresho katika
miundombinu, vifaa na vifaa tiba, kutoa mafunzo kwa Watumishi, Kusimamia
miradi ya IMF, Kupambana UVIKO -19 pamoja na Kusimamia upatikanaji wa
Sheria na Sera ya BIMA ya Afya kwa Wote.
“Katika kuboresha
huduma za afya Wizara inampango wa Ujenzi wa Hospitali za rufaa za mikoa
nane na za mikoa tano ambazo zitakuwa katika mikoa ya Njombe, Geita,
Simiyu, Songwe na mikoa mingine ni Mara, Singida, Shinyanga mpaka
kufikia mwaka 2025.”
Amesema kuwa katika Mkakati wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka 5 No.3
Hospitali ya Rufaa kila Mkoa na Huduma za Kibingwa kila Kanda zinahitajika.
Pia
amesema kwamba na mkakati wa Sekta ya Afya wa Miaka 5 kuanzia mwaka
2021 hadi mwaka 2026 wizara itahakikisha wanawaweka wadau wa sekta
pamoja ili kuchangia katika uratibu wa kutoa huduma za afya kwa ufanisi
zaidi.
Catherine amesema kuwa lengo la Wizara hiyo ni kutoa
huduma bora kwa kila mtu bila kujali hali na eneo alilopo. Wizara pia
inampango wa Kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza,
Kuboresha huduma za utafiti, ubunifu na uwekezaji katika sekta ya afya.
Katika
upatikanaji wa dawa na vifaa vya dawa na vifaa tiba amesema wataongeza
bajeti ya huduma za afya ambayo ni endelevu kiuchumi.
Amesema
maboresho ya Ujenzi wa vituo vya afya vyuo wizara itahakikisha itafanya
ukarabati na kuhakikisha hospitali 67 za wilaya zinajengwa hadi kufikia
2025."Hospitali za kanda mbili zilizojengwa ifikapo 2025 ambazo zitakuwa
katika mikoa ha Mtwara na Kigoma.”
Akizungumzia Ujenzi wa
viwanda vya dawa na vifaa tiba amesema wizara inajitahidi kupunguza
kuagiza nje dawa kwaajili ya kuhifadhi 'kusave' fedha za kigeni
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bi.
Catherine Sungura akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya Wizara na
waandishi wa habari kujadiliana na kushauriana masuala ya habari ili
jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakiwa katika
kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, katika kikao
hicho waandishi wa habari walijengewa uelewa kuhusu mikakati na
vipaumbele vya Wizara ya Afya katika kuwahudumia wananchi.Kikao hicho
kiliandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya Afya
Mwenyekiti
wa waandishi wa habari waliohudhuria kikao kazi hicho Vincent Kasambala
kutoka Upendo Media akizungumza jambo katika kikao kazi hicho
kilichowakutanisha waandishi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwandishi
wa ITV, Richard Steven akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi B,
wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari,
kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo,
Catherine Sungura, lengo ikiwa kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo
hicho kifanye maboresho ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu
afya.
Mkurugenzi
wa FullShangwe Blog, John Bukuku, akichangia jambo wakati wa kikao kazi
kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichoandaliwa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mwandishi
wa masuala ya afya na jamii wa Matukio na Maisha Blog, Veronica Mrema
akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi A, wakati wa kikao kazi kati ya
Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Catherine Sungura, lengo ikiwa
kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo hicho kifanye maboresho ili
jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.
No comments:
Post a Comment