Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekubaliana na Shirika la Umoja wa
Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) kushirikiana kutafuta namna na mbinu
bora zitakazoiwezesha Tanzania kuzingatia misingi ya Usawa wa kijinsia.
Makubaliano
hayo yamefikiwa (Aprili 06, 2022) Jijini Dar Es Salaam wakati wa Kikao
kati ya Wizara na Wadau wa Maendeleo kuhusu masuala ya Usawa wa
Kijinsia kutoka UNFPA.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula amesema,
Tanzania itahakikisha masuala yote kuhusu usawa wa kijinsia
yanazingatiwa kwa kuwapa fursa wanawake katika Nyanja mbalimbali
zikiwemo za uongozi na kiuchumi.
" Tunaongozwa na Miongozo
mbalimbali ikiwemo Dira ya Taifa …..na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) 2020-2025, hivyo, niwaombe tu, tuzingatie haya kwenye mipango yetu
Shabaha ni twende pamoja kwa matokeo chanya na ya haraka" alisema Dkt.
Chaula
Amesema jukumu kubwa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
ni kushirikiana na Serikali kutatua changamoto zinazoikabili jamii
ikiwemo ukatili wa kijinsia unaozidi kushamiri.
" Tunasikia kila
siku ukatili, mauaji sasa tushirikiane tuweke nguvu ya pamoja, tuwekeze
katika elimu kwa jamii, hii itasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili
" alisema Dkt. Chaula
Akichangia mada wakati wa kikao hicho
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum, Amon Mpanju amesema, Wizara itaendelea kushirikiana na
wadau kutafuta suluhu ya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Kwa
upande wake Mshauri wa masuala ya Kijinsia kutoka UNFPA Maja Hansen
amesema Shirika hilo liko tayari kushirikiana na Wizara katika
utekelezaji wa Mipango mbalimbali ikiwemo Mpango wa Taifa wa Kutokomeza
Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) 2017/2018-2021/2022.
Mkutano
kati Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
na UNFPA ni muendelezo wa vikao vya majadiliano na wadau mbalimbali kwa
lengo la kutatua changamoto za jamii.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, April 6, 2022
UNFPA KUCHAGIZA USAWA WA JINSIA NCHINI
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment