Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO),Mhandisi Frederick Kahimba
amesema wamebuni Teknolojia mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali
zitakazo wezesha watanzania kuagiza vifaa hivyo hapa nchini
Aliyasema
hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea
Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza na kuandika habari za Sayansi na
Teknolojia iliyofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
Tanzania(COSTECH)
Alisema kuwa Teknolojia hizo ni pamoja na
Majokofu ya kuhifadhi miili,Vitanda vya kujifungulia kinamama na
viteketeza taka katika hospitali
"Taasisi hii imekuwa ikibuni
vifaa mbalimbali vya hospitali na asilimia 80 ya vifaa hivi vinaagizwa
nje ya nchi,ni fursa kwa watanzania kuchangamkia hili kwa kuagiza hapa
nchini "alisema Kahimba
Injinia Kahimba alisema kuwa uwepo wa
vifaa hivyo hapa nchini itasaidia watanzania kujiajiri kwa kuanzisha
viwanda vidogo vidogo
Aliongeza kuwa wanashukuru COSTECH kwa
kuwawezesha fedha za kufanya utafiti kiasi cha shilingi milioni 128na
kati ya hizo milioni 65 walitumia kwaajili ya mtambo wa kusafishia
mafuta ya alizeti.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania TEMDO,Injinia Fredrick Kahimba akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uwepo wa vifaa mbalimbali vya hospitali vinavyotengenezwa na Taasisi hiyo
Fundi mahiri wa kutengeneza vitanda vya chuma kwaajili ya matumizi ya hospitali Flora Kweka akiwa katika majukumu yake.
No comments:
Post a Comment